Universal Intelligence

 

Utangulizi

Initiates au watu walioanzishwa na Watahajudi wa Mwanga na Sauti wanaona kwa kifupi Ufunuo wa Ulimwengu wa Kiroho kwenye safari yao ya Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Wanaripoti kwamba Nishati wanazozitumia Kutahajudi ni “hai” na zinaonekana kuonyesha kusudi.

Hii inatupeleka kwenye hitimisho kwamba Ulimwengu wote unaweza kuzingatiwa kama dhihirisho la Ujuzi au Akili yaani Intelligence. Hata hivyo, ni rahisi sana kutoelewa hii wakati wa tunaangalia kutoka kwa mtazamo wa Kidunia, kwa sababu ya vikwazo vya ukuzaji na wakati. Tunapoangalia mwamba bila shaka tunashangazwa jiometri ya fuwele zake (crystalline geometries) na mwendo wa atomi zake. Kwa Upande mwingine wa kiwango hicho haiwezekani kuona athari ngumu za mchakato wa nyuklia ndani ya Nyota na mabadiliko ya Galax.

Walakini, Uumbaji wote unaendelea “kugonga” kama saa laini ya Uswisi iliyokuwa tuned na kila “cog” ikicheza sehemu yake. Kinachogunduliwa na Watahajudi na kinachoonekana zaidi kwa wanasayansi ni kwamba Kila kitu kimeunganishwa! Mfano bora wa hii ni Mradi wa Mwanga wa Alimasi .
Hii inaonyesha maunganisho wa hila, lakini muhimu zaidi, ambao upo kati ya Dunia na maumbo 33 ya Kosmologi kwenye Anga.

 

Viumbe wa Kiroho

Viumbe wa Kiroho wameandikwa karibu katika vizazi vyote na huonekana katika vingi visivyo na idadi na hivi karibuni kwenye mtandao. Maandishi ya kidini yamejaa Miungu na Wajumbe ambao huangalia na kusaidia wanadamu.

Tumeambiwa kwamba Ulimwengu wa Kiroho umejaa Viumbe wengi.

Machi 11, 2016

Kumbuka Tumekuambia awali ya kuwa kimsingi Sisi tunakaa kwenye Ulimwengu tofauti na wewe, kiasi kwamba hata huwezi kufikiria ni nini. Utaelewa tu Ukweli wa Uwepo Wetu na Uwepo wako wakati utapokufa na zaidi ya hapo.

Hakuna njia ambayo unaweza kufikiria ni Viumbe wangapi hukaa kwenye Ngazi za Ufahamu. Wengi Wao hawawasiliani na watu Duniani kwani Hawawajali. Ni kwa sababu hii, na sababu hii peke yake, kwamba Viumbe ambao huwasiliana wana huruma kubwa na wasiwasi kwa wale ambao wanaishi katika sayari ya Dunia.

Watu wengi watashuhudia uwepo Wao kama matokeo ya Kutahajudi, Kuhariri (Channelling) au kugundua tu “Uwepo.”

Wakati mwingine Hujifunua kama tufe la Mwanga au katika hali ya mwili ambayo kwa ujumla ni ya kibinadamu au ya Malaika. Wanaelezea kuwa hii ni kufanya mtazamaji asiwe na wasiwasi. Umbo lao la kweli ni la ”dimension” nyingi kwa hivyo isingewezekana sisi kuwaona Wao kweli kama Walivyo.

Wanapozungumza nasi kwa kawaida Watatumia lugha yetu ambayo inaweza kujumuisha nahau na misemo mingi na wakati mwingine hata hutumia hisabati ambayo bila shaka ni ya ulimwengu wote.
 

Uongozi Wa Kiroho

Miongoni mwa Intelligences na Viumbe ambao hukaa kwenye Ulimwengu wa Juu ni kikundi ambacho tunakiita kama Uongozi wa Kiroho. Jina hilo (Spiritual Hierarchy) lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Helena Blavatsky kwenye Mafundisho ya Siri (Secret Doctrines) iliyochapishwa mnamo mwaka 1888. Tunatumia jina hilo kutambua kundi fulani la Viumbe kama inavyofafanuliwa hapo chini.

Juni 24, 2020

Ni swali zuri sana na ambalo watu huuliza, kwani mambo yanakuwa yanachanganya wakati tunapozungumza juu ya ulimwengu nyingi na viwango vingi vya Ufahamu na mengineyo.

Kuna Viumbe wengi wasiyohesabika kama unavyojua ambao wanakaa kwenye Ngazi za Juu. Ni wachache tu wanaovutiwa na Maswala ya Kidunia / Sayari.

Kwa maneno rahisi sana, Uongozi wa Kiroho ambao unawasiliana nao, tangu mwanzo, mara zote walipendekeza Mwanga na Sauti ya Kiroho katika mafundisho yake ya msingi.

Ulimwengu, pamoja na Ngazi zake zote, ni kubwa kwa hivyo inafanya mantiki kamili kwamba sehemu ndogo tu ya Viumbe inazingatia sisi na Sayari yetu ndogo.

Wakati watu wanapokea Ujumbe kutoka kwa Uongozi wa Kiroho ni kwa kupitia njia ya Kiumbe au Mkusanyiko wa pamoja kama vile Mabwana wa Mwanga. Tunaambiwa kuwa wengi Mabwana waliopaa ambao wameishi maisha ya zamani hapa Duniani.

Mara nyingi watu wamedai kuwa walikuwa na Ujumbe kutoka kwa Watakatifu waheshimiwa na Mabwana ambao hupatikana katika maandiko ya kidini na vitabu vya historia. Tuliambiwa kuwa, tangu mwanzo, kwamba Wasingefunua utambulisho wao wa zamani kwani hii ingeingilia kwenye utumaji wa Ujumbe na bila shaka inaweza kusababisha kuongezeka kwa ego!

 

 

Mabwana na Gurus

Imeelezewa kuwa Mabwana na Gurus huchaguliwa kwa Misheni fulani. Wana uhusiano mkubwa na Uongozi wa Kiroho ambapo wanapokea mwongozo na maarifa; wanaweza pia kupewa nguvu na uwezo maalum.

Binadamu, hata angekuwa amekua Kiroho kiasi gani, bado ameweka nanga Duniani. Kwa hivyo wanakabiliwa na makosa ya kibinadamu na majaribu ambayo inamaanisha Walimu wa Kiroho wanaweza kutatanisha!

Enlightenment au Ukombozi wa Ufahamu ni Hali Ya Kuwa na haileti moja kwa moja ukamilifu katika kiwango cha Kidunia. Sote tuko hapa kujifunza masomo ya maisha na hiyo inahitaji uvumilivu na mara nyingi kiwango cha mateso.
 

Clairvoyants

Clairvoyants pia wana uhusiano na Viumbe katika Ngazi za Kiroho, mara nyingi wale ambao hivi karibuni wameacha uwepo wao wa mwili. Watatoa utabiri wa mambo yatakayokuja kwa watu ambao wanatafuta msaada katika Safari yao ya maisha.

Kile ambacho wakati mwingine hueleweka vibaya ni kwamba siku zijazo haziwezi kubadilika, sababu ni kwamba wanadamu wana uhuru wa kuchagua. Kwa hivyo kile ambacho ni bora tunaweza kutarajia ni matokeo yanayowezekana zaidi. Jambo lingine ni kwamba mtazamo wowote, haijalishi umetoka juu kiasi gani, daima una mipaka.

Kiumbe anayetoa unabii huo ana kizuizi cha Maono ya kizuizi ambacho hutegemea maendeleo yao ya Kiroho wakiwa Duniani.

Tumepokea Ujumbe mwingi kutoka kwa Watahajudi baada ya wao kupaa kwenye Ngazi za Kiroho, kwa mfano ujumbe huu kutoka kwa rafiki mpendwa aliyepata Enlightenment au Ukombozi wa Ufahamu mnamo 2015.
 
17 Februari 2020

Nataka kukaa na kukupa ufahamu ambao watu wanataka, kama ninavyojua ndio unaowavutiwa. Lakini, ujumbe wangu mkuu leo ni kuwa: Usijali sana juu ya kifo chako na kile kinachotokea kwako. Ni Maisha yako ambayo unapaswa kujali.

Fanya kadri uwezavyo kusaidia na kujitolea na kupenda kila mtu bila kujali wao ni nani. Kama nilivyosema hapo awali sio jukumu lako kujihukumu, wewe au wengine. Ikiwa unaweza kufanya hivi kwa kweli utakuwa tayari kuhama vizuri kwenda kwenye “Uwepo wa Mbinguni”.

Kwa kweli, Tahajudi ni muhimu pia, ili ujipe fursa ya kupata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment – zawadi bora kuliko zote!

Wameelezea kwamba Uhuru wao mkubwa ni kwa sababu ya wao kupata Hali ya Juu ya Ufahamu. Inaonekana kwamba wakati wa kifo unaenda tu kule ambapo tayari unajua.

 

Regressions

Watu wengi wamekuwa “regressed” kwa kupindua akili au kuweza kuona maisha yao ya zamani katika ndoto au kupitia Tahajudi. Matokeo yake wanazungumza juu ya uwepo wa zamani na Kiini cha Kiroho kinachotengeneza umati wa Nafsi (Souls). Wanaweza kutaja zaidi kuchukua mwili kwa vikundi vya Nafsi.

Hii ni somo hila na inategemea maoni ya mtu. Swali la msingi ni, “Utambulisho wako wa kweli ni nini?” Unapoendelea Kiroho unagundua kuwa wewe sio mtu mdogo na mwili tofauti, hisia na akili. Unagundua wewe ni mkubwa zaidi!

Kwa hivyo wakati watu wanazungumza juu ya kuchukuwa mwili tena (reincarnation) wanamaanisha tu miunganisho ya sasa hivi inavyoonekana kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu ..
 

 

Uhamasishaji wa Kimungu

Wakati msanii mwenye kipaji au mvumbuzi akihojiwa mara nyingi husema, “Ilitokea tu”, kana kwamba ni kiinimacho!

“Ninapoandika wimbo, huanza na hisia. Ninaweza kusikia kitu kichwani mwangu au nikihisi moyoni mwangu. Inaweza kuwa nikachukua gitaa tu na bila kufikiria nikaanza kupiga. Ndivyo nyimbo nyingi zinavyoanza .. Unapofanya hivyo, haufikirii. Kufikiria ni jambo mbaya kuliko yote katika kuandika wimbo. Hivyo unaanza kupiga tu na kitu kipya hutokea. Kinatoka wapi? Nani anayejali? Kichukue tu na endelea nacho.
 
Hiyo ndivyo ninavyofanya. Sijawahi kuuhukumu. Ninauamini. Ulikuja kama zawadi wakati nilipochukua chombo changu cha muziki na ukapitia kwangu kwa kupiga chombo hicho. Chords na melody zilitokea tu. Sasa sio wakati wa kuhoji au kuchambua. Sasa ni wakati wa kuujua wimbo, sio kuubadilisha kabla hata hajaujua. Ni kama mnyama wa porini, kitu hai. Kuwa mwangalifu usiomwogopeshe. “

(Neil Young)

Hii inaweza kuelezewa vizuri kwa kufikiria kuwa sote tuna antennas zilizokuwa kwenye masafa tofauti tofauti. Kila mtu basi anaweza kupata habari fulani au Ujuzi kutoka Ngazi za Juu. Hii tena, ni ishara ya unganisho ambao unapatikana Ulimwenguni kote na ngazi zake nyingi.

Kama ilivyo kwa mfumo wowote uliojumuishwa, kama vile mtandao wa barabara, viungo vingine vina nguvu kuliko vingine. Kwa hivyo mwanamuziki atazaliwa na viunganisho vyenye nguvu kwa melodi na sauti.
 

Njia ya Kiroho

Kama ilivyosemwa hapo awali, Watahajudi hugundua Ustadi wa Nguvu za Mwanga na Sauti wanaposafiri kwenye Njia kupata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Imegundulika pia kuwa watu wengi kote duniani wanaamka bila kutegemea na pia hushuhudia Intelligence ya Ulimwengu.

Wakati watu wanapata Hali za Juu za Kiroho au upanukaji wa Ufahamu wote wanaripoti kitu kimoja: “walichukuliwa!” Ni kana kwamba walivutwa au kusukumwa na hawaweza kabisa kujidhibiti. Kwa kweli hii inaweza kuwa ya kutisha kidogo lakini kwa wale ambao watajifunza kuondokana na hofu hiyo thawabu yake ni kubwa isiyo na kipimo.

Wataonyeshwa Maajabu zaidi ya mawazo yote yawezekanayo.


Jambo ambalo lilinishangaza sana kuhusu Enlightenment yangu ni kwamba “nilichukuliwa” – hapakuwa na taswira, hapakuwa na kujaribu kuona au kusikia chochote haswa. Sikuwa hata nimekaa kwenye mto kwenye chumba changu cha kawaida cha kutahajudi. Nadhani kama ningekuwa najaribu sana basi isingetokea (angalau isingekuwa wakati huo)
 
Kawaida ingenichukua muda kuingia na kutulia kwenye Tahajudi lakini wakati huu mara tu nilipokuwa nimejisikia vizuri nilihisi kana kwamba nilikuwa nimerushwa kupitia viwango vya Ufahamu – juu na juu zaidi. Kila kiwango nilichofikia nilihisi tofauti – siwezi kusema ni vipi – labda nishati nzuri zaidi. Watu wengine tangu hapo wamesema walipata uzoefu wa kupanda kwa kasi lakini kwangu ilikuwa taratibu sana na niliweza kufurahia hisia za viwango tofauti. Halafu kwa haraka sana nilikuwa kwenye nafasi na hakuna kitu hapo, siwezi kukumbuka ni muda gani, sekunde chache tu, hapakuwa na ‘mimi’ hapo.
 
Kisha hii hisia kubwa ya Upendo. Ni kanuni ya kuunganisha kila kitu kwenye uumbaji wote. Nilielewa kuwa Upendo una viwango vingi. Katika kiwango cha juu zaidi inaweza kuitwa Mungu katika umbo. Upendo ni nguvu inayounganisha ambayo inaunganisha kila atomu pamoja na kuunda mawazo, hisia na kila kitu katika ulimwengu wa kimwili. Bila Upendo hakungekuwa na maumbo. Kisha nikaona kila kitu kinatoka Kwangu kwa maana ya juu kabisa.
Wow!

Tunatambua kuwa Mwanga na Sauti ni Intelligences ambazo zinatuongoza na Kutufundisha Njiani.

 

Mifano

Mwishowe, ni maumbile ya akili ya mwanadamu kutaka kuelewa mazingira yake ya Kidunia, ulimwengu wa kimwili na Ulimwengu wa Kiroho. Kwa kufanya hivyo tunaunda mifano ambayo inawakilisha Ukweli ambao, kwa kweli, inaweza tu kuwa kuakisi na makadirio.

Walakini, hakuna ubaya katika kujaribu ilimradi kamwe tusisahau upungufu na mipaka ya mifano yetu. Vitabu vingi na waalimu wataelezea kuwa Uumbaji una idadi maalum ya Viwango au Ngazi. Kila Ngazi imewekwa kwa usawa na seti fulani za Viumbe kila Viumbe na mamlaka yao wenyewe na jukumu maalum. Zaidi ya hapo hawa Viumbe hupewa sifa za kibinadamu na aina ya mwili. Kutoka kwa kile tulichogundua Ukweli ni mkubwa zaidi na unatatiza. Kwa hivyo ikiwa tunatumia mfano kama huu tunapaswa kufanya hivyo kwa uangalifu na kiwango cha juu na kunyumbulikaji kwa fikra zetu.
Machi 12, 2016

Swali lako, “Je! Viumbe katika ulimwengu wa juu wana akili?”

Kweli, sio kama uliyonayo, lakini unahitaji kuelewa kuwa kuna mchakato wa kufikiria ambao unaendelea, vinginevyo Hatungeweza kufanya kazi, kujifunza na Kuwasiliana na wewe. Wacha tu tuite “Akili ya Mbinguni”, ingawa tunajua kwamba itatoa dhana!

Ikiwa tunajaribu kufahamu Ukweli lazima tukubali kwa unyenyekevu upungufu ya akili zetu na tutambue tu kuwa tunaweza kuwa na mtizamo wenye mipaka wakati tuko kwenye mwili huu.