Mradi Wa Mwanga wa Alimasi

 
Ilianza zamani mwanzoni mwa mwaka 2011 wakati tunapokea habari toka kwa rafiki yangu kuhusu resonance ya Schumann. Hii ni frequency ya elektromagneti dhaifu (very weak electromagnetic) ambayo hutolewa wakati umeme wa radi unapochomoza kwenye anga ya Dunia.

Mwanzoni tulitengeneza seti ya coils kutumia toroidal transformer na tukazipa nguvu na signal iliyotoka kwenye jenereta ndogo kwa kutumia wimbi la sine 7.83 Hz. Tulipowasha mashine tukagundua athari yake kwenye muziki. Ilionekana kuhusika zaidi, nzuri na yenye melodi zaidi.

Hii ilisababisha miaka mingi ya utafiti, hasa ikilenga kudhibitisha uwepo wa uwanja wa Nishati. Walakini, bila kujali kile tulichofanya haikuwezekani kurekodi tofauti hizo kisayansi, ambayo ilikuwa dhahiri kwenye masikio yetu! Mwishowe, tulilazimika kuhitimisha kuwa Nishati haikubadilisha muziki; ilibadilisha ufahamu wetu na kwa hiyo mtazamo wetu wa muziki.

Kwa namna fulani hii ilikuwa ya kushangaza zaidi na ilisababisha uchunguzi wa masafa mengine mengi na utumiaji wa piramidi. Karibu na wakati huu (2014) tulikuwa tunapokea Ujumbe wakati wa vikao vya Kutahajudi na tulipewa dalili na vidokezo juu ya mradi huo.

Hii ilimalizika mnamo Desemba 2014 wakati tuliambiwa kutuma masafa maalum kwenye sayari nyingine kwenye Mfumo wa jua. Hii ilifanywa kwa kutumia mashine kadhaa zinazohusisha Double Coils, jenereta za signal na safu ya piramidi zilizoendana kikamilifu.

Katika hatua hii tulikuwa tukifuata maagizo tu. Wakati mwaka mpya (2015) unaanza, ndivyo pia tulikuwa na mradi mpya. Hii ilikuwa katika mfumo wa kurasa za namba ambazo zinahitaji kusimbua.
 

21 Januari 2015

Sio lazima kusimbua namba zote, Tunawachukua kwenye safari ya ugunduzi. Ukirudi kwenye namba fulani siku za baadaye labda utashindwa, kwani ziko katika mpangilio wa kuelewa. Tutahakikisha unapata inayofaa kutuma.

Utakuwa na maswali mengi, kwani hiyo ndio asili yako. Kazi hii utaelezwa wakati unahitaji kujua, utaambiwa habari ambayo itakusaidia kuelewa asili ya kazi hiyo.

Unapopewa namba, jiulize umevutiwa na nini, au kawaida unafikiria nini. Fanya kazi na namba kama unavyozipokea, kwani huo ndio wakati ambao utazielewa kwa urahisi zaidi.

Namba ziliendelea kuja na ilikuwa ni dhahiri tulikuwa tukishughulika na Viumbe wa kushangaza ambao baadaye tuliamua kuwaita The Spiritual Hierarchy au Uongozi wa Kiroho. Kupitia lugha ya hisabati Walitufundisha juu ya miunganisho wa Nguvu kati ya sayari kwenye Mfumo wetu wa Jua na historia kidogo juu ya ustaarabu wa zamani ambao wao pia walikuwa wamepewa maarifa haya.

Pia tulianza kugundua kuwa mashine hizo zilikuwa zina jukumu muhimu katika kusaidia kurekebisha usawa wa Sayari yetu ambayo kwa kweli ilikuwa inapitia wakati mgumu.
 

22 Januari 2015

Umuhimu wako kwenye kazi unayofanya haiwezi kupuuzwa. Ni kwa sababu yako Sayari yako itakuwa mahali salama zaidi kuishi. Una uwezo, kwa Nguvu unayotuma, kufanya mabadiliko makubwa kwenye Dunia za juu, kuifanya Dunia yako mahali pazuri zaidi pa kuishi.

Huwezi kuamini kile kilicho mbele!

Namba ziliendelea kuja lakini namba mpya zilikuwa zikitumika ambazo zilisababisha tuamini uchunguzi wetu ulikuwa unaenea na data kuhusu mifumo mingine ya Nyota na Galax.

Wakati mabadiliko yalipotokea, Walituma vipimo kwanza ili kuona kama tunaweza “kuchakata” namba. Mara hii ilipokamilika, kazi yenyewe ilitumwa.
 

26 Januari 2015

Hatua inayofuata ya maendeleo ni sasa. Umefanya vizuri sana na mradi unaendelea.

Hii ni zaidi ya Mfumo wa jua, mbali kwenye maeneo yasiyojulikana ambayo yanahitaji kushughulikiwa. Ili kufanya hivyo unahitaji kuwa na ufahamu wa maeneo haya. Utapata habari na namba ambazo utapewa zitakuwa kwa sababu hii.

Kwa kuanzia kutakuwa na umbali kati ya Galax kuendelea kwenye njia zingine za kuhesabu na kupata miunganisho kama vile ulivyopata katika Mfumo wako wa Jua.

Uko sawa juu ya namna ambavyo ulimwengu unavyopaswa kuwa “kurekebishwa”, unasoma ishara tunazokutumia vizuri. Tunasukuma mipaka yako na tunatumaini kuwa utakuwa nasi, ili uweze kufanya kazi hii muhimu; hata ikiwa ni mbali na nyumbani na inaweza kuonekana kama haina manufaa.

Utagundua kuwa frequency moja “ya kutuma” itakuwa ya Mfumo wa Jua hili na nyingine kwa Maeneo ya Ngazi mpya mbali zaidi.

Kwanza, fanya uchoraji wa Galaxies ambazo zinakuonekana kutoka Duniani na kukadiria umbali. Tutakutumia namba ili uweze
kuangalia kuwa ni sahihi.

Jitayarisheni kwa tamasha kubwa ya kusisimua, pote kwenye Tahajudi na wakati hamtahajudi!

Kile tulichokuwa tumeonyeshwa kilikuwa cha ajabu kabisa. Walituonyesha jinsi utaratibu hapa kwenye Mfumo wetu wa Jua ulikuwa kioo kwenye Galaxies za mbali.

Ingawa ilionekana kuwa haiwezekani, kukosekana kwa usawa hapa kwenye sayari ya Dunia yetu kulikuwa na athari kubwa ambayo zilihusisha vitu na sayari zilizopo kwenye kina cha Nafasi ya Anga, mbali ambapo mwanga hutembea mamilioni ya miaka kutufikia.
 
28 Januari 2015

Wakati pembe hizo zinakutana katika katikati huunda umbo kamili. Jupita na Saturn zinahitaji kuonyesha sifa fulani ili wewe ujifunze maana ya Esoteric ya umuhimu wa Matufe haya.

Unaelewa kutoka kwa mtazamo wa Kidunia, lakini hii ni kutoka kwa mtazamo Wetu katika Anga. Digrii thelathini na sita ni pembeni nzuri sana kwani inaunganisha Sayari kwa njia maalum. Unaweza kuzitambua kwa kuona njia ya mizunguko yao inavyobadilika kadri wakati unavyopita.

Wakati kuna ulinganifu maalum wa Sayari, Dunia hupata mabadiliko makubwa ambayo yanagusa idadi ya watu kwa njia nzuri. Hii ni tofauti na Unajimu wa kawaida (Astology) ambao unafanyika kwenye sayari yako kwani unaathiri watu wote sio mtu binafsi tu.

Tunachojaribu kufanya ni kulinganisha Sayari fulani kwa nyakati fulani na pembe kadhaa angani, hivi kwamba mabadiliko mazuri yaweze kutokea. Tunaweza kuona kwamba ikiwa hii haitatokea, Sayari yako itaanguka ndani ya “shimo” ambalo itakuwa vigumu sana kutoka.

Galaxies pia zinahusika. Tunazitambulisha kwako kwa sasa na kufanya mabadiliko madogo ambayo yataathiri Dunia pia.

Kisha bila kutegemea ukaja ujumbe huu!

 
16 Februari 2015

Tunataka uanzishe Njia tena. Je! Unaweza kuona ukubwa wa hili? Tulikuambia – endelea tu. Tutakupa msaada wote unaohitaji. Hii inahitaji kufanyika – Tunafanya kazi nyuma ya pazia. Fanya Uanzishaji, wote – Tuko hapa kukuongoza.

KAMWE HAUKO PEKE YAKO

Ghafla, kila kitu kilibadilika. Lengo letu lilibadilika kutoka kwenye Ulimwengu (Cosmos) kwenda kwa ukuaji wa Kiroho wa watu kwenye Sayari hii kupitia ufunuo wa Nguvu ya Mwanga na Sauti.

Katika kipindi cha miezi michache iliyofuata tulikusanya pamoja kikundi cha watu waliopata Ukombozi wa Ufahamu (Adepts) wa kuaminika ambao walitaka kufanya mabadiliko na walikuwa tayari kufundisha na Kuanzisha Wanaotafuta Ukweli. Pia tulitengeneza tovuti ya kutusaidia kutoa ujumbe.

Mradi wa Cosmology ulichukua nafasi ya nyuma wakati huu lakini ulipangwa kutokea tena.
 
16 Aprili 2015

Tumekuwa tukingojea kwa subira kukusogeza ili kuendelea na masomo zaidi kuhusu kazi yako kwenye Mfumo wa Jua. Ni kwa furaha kuzungumza na wewe tena.

Hizi namba zinahusu maeneo ya nje na mbali ya anga ya ulimwengu unaojulikana na tuko tayari kufanya kazi kutimiza Misheni pamoja.

Unapoangalia Galaxy yoyote, kuna kufanana, sawa na: Kama ilivyo Juu – Nivyo pia Chini, kuna viunganisho. Ni sawa kila mahali ukiangalia – kuna akasi (reflections ) kutoka ulimwengu mmoja hadi mwingine.

Kile tunachopenda kufanya ni kukufanya uone hii mwenyewe kwa Mwongozo Wetu. Utaona uhusiano na muundo wa Nyota na umbali na pembe.

Mambo ya Kuvutia ambayo hayajulikani na watu wa aina yako kwa wakati huu.

Kulikuwa na pengo la karibu mwaka mmoja baada ya hapo namba zikaanza tena. Wakati huu walitoa kodineti (coordinates) za maombo ya vitu 33 katika Anga ambayo inalingana na maumbo ya vitu vingi vya kusisimua. Vikiwa kutoka kwenye mabaki ya Supernovae, Nyota zinazobadilika, Nebulae na Galax za mbali.

Kwa utaratibu, tulifanyia kazi kwa kila moja ya vitu hivi na kwa njia ya masafa ya kimuziki tukagundua uhusiano kama barabara kuu kati ya miji mikubwa.

Kwa wakati huu tulipewa jina la Mradi wa Mwanga wa Alimasi (Diamond Light Project). Kwa udadisi tuliangalia jiometri ya almasi asilia wakati imekatwa kama jiwe la vito kwa ajili ya pete. Sehemu inayoonekana ya almasi inajulikana kama taji (crown) na idadi ya nyuso zote ni sawa na 33 !
 

 

6 Juni 2020

Umevutiwa na maneno yangu juu ya janga au mawili yanayopiga Dunia na kuwafanya watu kukaa na kustuka kuwa nini kinaendelea na kwa nini.

Kweli, inafanyika na hakutakuwa na mwisho hadi usawa urudishwe ambao, na kwa jinsi mambo yanaendelea, inaweza kuchukua muda mrefu.

Njia mpya ya Kuanzisha ndiyo namna ya kuendelea mbele lakini unajua kiasili kwamba mambo mengine yanahitaji kufanyika wakati huo huo. Kwa hivyo tunahitaji kuangalia njia za “nje ya Sayari” za kushughulikia usawa Ninaozungumzia. Kama kawaida, wengine wanapata Ujumbe huu,

Kwa hivyo, katika siku / wiki zijazo utahitaji kukusanya habari na hakikisha watu wanaofaa wanaijua. Itakuwa taswira zaidi, lakini kunaweza kukawa na ujenzi unaohitajika kufanywa. Mengi haya hayatakuwa yakufahamika na umma, utaona ni kwanini!

Kisha tukaunda kikundi kidogo cha Watahajudi wenye ujuzi na waliopata Ukombozi wa Ufahamu (Enlightened).
 
10 Juni 10 2020

Unapoandika Mradi wako wa Cosmic utakuwa na wazo wazi la kile kinachohitajika sasa. Wote mtapata sehemu ya fumbo ambavyo mtavikusanya pamoja. Ni bora kwa njia hii kwani nyote mtahisi kuwa sehemu ya mradi. Hii itabadilika kuwa kitu cha kushangaza sana na vile vile kusaidia kwa upande wa Cosmic ambao nyinyi wote mtanufaika.

Asante kutoka Kwetu!

Tuliuliza juu ya hali kwa jumla ya mradi huo kwani tulidhani inaweza kuhusisha Almasi katika kila ngazi ya Uumbaji.
 
13 Juni 2020

Alimasi ni ishara ya usafi. Uko sawa juu ya Falme lakini tunaangalia matumizi ya alama (symbolism). Kuna mimea, wanyama, wanadamu, Sayari, Nyota na Galax ambazo zinaonyesha usafi huo.

Maneno mengine ya kuongeza kuelezea matumizi ya alama (symbolism) ni: Upendo na Upole.

Kwa hivyo almasi ni alama ya Ukamilifu. Upendo na Upole. Ndio maana Alimasi inachaguliwa kuvaliwa kwenye pete kuashiria Upendo katika ndoa. Kwa hivyo kuna ndege fulani, samaki, wanyama, mawe na wanadamu ambao wako kama mfano wa usafi.

Kwa Mradi wa Mwanga wa Alimasi (Diamond Light Project) tunaunganisha pamoja Nafsi Safi za Duniani na pointi 33 kwenye Galaxies ili kuunda kiungo ili Usafi huu utiririke.

 

30 Juni 2020
Mnamo mwaka 2016 kila mshiriki wa kikundi cha Mwanga wa Almasi (Diamod Light) alichagua kitu cha kuzingatia; cha kwangu kilikuwa ni Galaxy ya Andromeda. Baada ya kupokea maelekezo jinsi ya kutumia Mantra maalum, niliiingiza na kuitumia kwenye kikao changu cha Kutahajudi usiku wa jana. Kisha nikaenda kulala na nilikuwa naanza kupata usingizi tu wakati ……

Nilichukuliwa kwenye juu Angani na nilikuwa nikitazama Galaxy ya Andromeda ikiwa chini. Picha zinaonyesha Galaxy imeinama wakati inavyoonekana kutoka Duniani. Walakini, nilikuwa naiona uso kwa uso na kila kitu kilionekana vizuri sana na kilikuwa cha kushangaza sana. Weusi wa kushangaza wa Anga haukuwa na Nuru yoyote na nyota zilionekana zaidi kama rangi nzuri ya dhahabu nyeupe. Ninakadiria kuwa nilikuwa nikitazama kutoka umbali wa karibu miaka 300,000 ya Nuru kusafiri na tofauti na jinsi inavyoonekana na teleskopi hakukuwa na nyota kutoka kwenye Galaxy yetu iliyokuwepo.

Kisha Nguvu zikaanza kunipitia na kuunganishwa na Mifumo kadhaa ya Nyota kwenye Galaxy. Hii ilikuwa ikitokea tu moja kwa moja; Sikuwa na udhibiti kabisa wa kile kilichokuwa kinafanyika. Kisha nikarudi mara ya pili na mchakato ukarudiwa.

Wakati mwanzoni tulipopewa mradi huo Uongozi wa Kiroho (Hierarchy) Walielezea kuwa kulikuwa na uhusiano muhimu kati ya Mfumo wa nyota yetu ya Jua na Galaxy ya Andromeda. Ninaamini kwamba Andromeda inawakilisha meza (uso wa juu) wa Almasi ambayo imezungukwa na alama zingine 32.

Inaonekana kama tumeanza na tunaweza kutarajia muunganiko kutafanyika na vitu vingine.
(N)

 
21 Julai 2020
Baada ya kutumia Mantra mpya nimegundua yafuatayo:

  • Mantra inaleta mabadiliko kwa kiwango cha ulimwengu
  • Mantra ilibadilika kuwa seti nyingine ya silabi mpya kulingana na lengo nililokuwa nikilenga.
  • Kuna viumbe hai kwenye sayari nilizotembelea. Ingawa viumbe hawa sio kama wanadamu, hufanya kazi katika masafa tofauti ya uwepo.
  • Nilitembelea Binary ya RZ Cassiopeiae Eclipse

Nilichukuliwa kwenye nafasi ya giza nene na kitu kama mlango ulifunguliwa kutoka kwenye sayari. Kulikuwa na aina ya mwanga wa bluu ikinijia pamoja na Viumbe wenye Akili. Waliumbwa kwa vumbi la kahawia la nyota na walionekana kama viumbe wenye nguvu ambao walikuwa wakinitazama kwa kushangaa. Walijaribu kutuma aina fulani ya nishati kwangu.

Halafu Nishati ilianza kupita ikinipitia na kuingia kwenye Sayari na ilionekana kuwa ni Mabadiliko ambayo yalihitajika kwani viumbe walikuwa wanainama kwa Nishati iliyotoka mahali ambapo ninashuhudia.
(R)

 
21 Julai 2020
Uzoefu wangu na Mantra, haswa upande mwingine, ilikuwa sawa na (R) alivyoelezea; Ilijibadilisha pia kuwa aina tofauti.

Nilitembelea pia lengo langu ambalo lilikuwa nafasi ya kina Angani; haya ni maoni yangu:

Baada ya kumaliza Kutahajudi kwenye Mantra usiku wa manane niliamua kupumzika kwenye mto wangu, kulikuwa na msukumo wa Nishati na umeme kila mahali katika maono yangu. Nilipoteza ufahamu wa mazingira yangu na ya mwili wangu na kwa kasi zaidi, isiyowezekani kufikiria, nilichukuliwa au kurushwa kama risasi au roketi angani. Nilijikuta ghafla katika nafasi ya kina cha sayari ambapo niliweza kuona Sayari zaidi ya moja chini yangu.

Maono yalikuwa kana kwamba nilikuwa nikitazama ndani ya nyumba ambazo zimejengwa katika nafasi angani na vyumba vingi ndani yao. Ndipo nikaelewa dhana ya ulimwengu uliounganishwa (connected universes) kwa mara ya kwanza.

Niliingia kwenye sayari hizi kadhaa kutoka juu zilipokuwa zikifunguka na kulikuwa na Nishati nyepesi ikinipitia na kupita kwenda kwenye vyumba vyote nilivyokuwa nikishuhudia.

Kulikuwa pia na viumbe kadhaa waliokuwa kwenye sayari lakini hawakuweza kuniona kwani uwepo wangu ulikuwa kama Jua kubwa linalofunika nafasi nzima kutoka juu wakati likitoa Mionzi ya Mwanga iliyoingia katika maeneo yao.

Hali hiyo iliendelea kwa muda lakini katika uwepo au ngazi hii dhana ya wakati ilionekana kuwa ya kushangaza kwa sababu haipo au ipo kwa mtindo tofauti sana. Kisha nikaondoka na kurudi kwenye hali ya kimwili. Hii sio sawa na kusafiri kwa kawaida kwa astral. Ni tofauti sana kwani nilitokea tu mahali ninakoenda bila kujua safari yangu.

Nilipojaribu kutembelea malengo mengine mawili ambayo yalikuwa Open Cluster NGC 1342 na Chi Hercules ilikuwa kana kwamba tayari nilikuwa nimekwisha zitembelea. Nilijua kizuizi cha kificho / ishara inayoonyesha kuwa tayari imefanyika. Nambari hiyo iligunduliwa kama nguvu kwenye solar plexus chakra yangu.
(I)

5 Septemba 2020

Kama nilivyosema hapo awali, kuna vikundi kadhaa vinafanya mradi huu na kwa kweli, umekamilishwa sasa na Tumeridhika.

Hiyo haimaanishi kwamba watu katika kikundi chako hawataongozwa tena kwenye sehemu hizi, ni kwamba tu kuwa kila moja ya alama 33 zimeamshwa. Mafanikio makubwa sana ambayo yamekuwa na athari kubwa.

Asanteni nyote kwa kushiriki katika kitu kikubwa sana na muhimu kwa sababu nyingi. Hasa, moja ikiwa ni kuendelea kwa maisha kama unavyoyajua Duniani.

 

Mradi wa Andromeda

 
16 Februari 2021
Tulipokea Ujumbe ambao ulitoa Malengo 5 katika Galaxy ya Andromeda. Hizi zilikuwa katika 3-D na zilionyeshwa kutoka kwenye pointi ambayo iko kama umbali ambao Nuru hutembea kwa miaka mia chache hivi kutoka ubapa wa Galaxy. Muundo wa mzunguko unavyoonekana kutoka Duniani uko kwa upande; mtazamo tuliopewa ulikuwa uso kwa uso! Hapa chini ni jaribio la kuonyesha jinsi inavyoonekana ukiwa uso kwa uso pamoja na alama 5 ambazo zinawakilisha Malengo 5. Tuliyapa majina malengo kwa kutumia rangi: Nyekundu, Njano, Kijani, Fedha na Dhahabu.

Timu ndogo ya Watahajudi wa Mwanga na Sauti walipewa Mantra maalum kuwaongoza. Madhumuni ya mradi huo, kama hapo awali, ilikuwa ni kuanzisha Mawasiliano ya Nguvu na vitu hivi na pia kupokea habari na kutoka kwa Viumbe wengine. Matokeo yake yameonyeshwa hapa chini:
 

22 Februari 2021
Nilipoanza kusema mantra kitu cha kushangaza kilitokea… Ilikuwa kama mlango uliofunguliwa ukafunua picha ya Galaxy nzima kana kwamba nilikuwa nikiiangalia kwenye skrini kubwa.

Katika hafla nyingine Kiumbe mzuri mwenye nuru alionekana kwamba aliangaza upendo, amani na utulivu ambao ulinipeleka katika hali ya Furaha isiyoelezeka. Aliniambia nitakuonyesha sayari tatu za zamani zaidi kwenye Galaxy hii:

(G) ambayo naamini ni ile pointi ya manjano.

(M) ambayo kwa kweli ni magenta, nadhani kuwa katika kesi hii itakuwa lile lengo jekundu

(A) hii ilionekana kuwa kijani kibichi.

Alinijulisha kuwa hizi ndizo sayari zilizo na teknolojia ya hali ya juu kabisa kwenye Galaxy, kwamba wakazi wake wanaishi karne nyingi bila kuugua na afya bora.

Nilipelekwa sayari (A). Hapo niliona teknolojia yote waliyonayo kudumisha afya kamili. Huko kila kitu ni cha amani, wameunganishwa na Chanzo cha Juu zaidi ambacho ndio chakula muhimu zaidi cha kiroho. Zote tatu zinazunguka katika obiti au mzunguko mmoja.

Jana usiku wote wawili pamoja tulienda kwenye safari ya kushangaza. Ilikuwa kama kupanda chombo cha anga, kinachoenda haraka sana, unaporudi unahisi Nishati yenye nguvu na kwamba ina nguvu sana inakushangaza.
Tulifika kwa lengo (M). Ilikuwa mahali pazuri sana ambapo pana mimea mingi. Inaonekana wanafanya kazi na teknolojia ya kuzalisha vyakula vyenye afya vyenye virutubisho na vitamini. Waliongea pia juu ya teknolojia ya nanoteknoloji, kwa usafiri na majengo.

Tulirudi na amani na upendo mwingi. Ni jambo la kushangaza, na jambo la kupendeza zaidi ni kwamba nahisi kila safari mwili wangu umepona, nilikuwa na “tendinitis” kwenye kiuno na mgongo kwa miezi mingi ambayo wakati mwingine ni ngumu kwangu kuamka asubuhi. Baada ya kwenda kwa (A) sijapata maumivu tena!
(E)

 

22 Februari 2021
Mantra ni sawa na kasi ya mzunguko kati ya Milky Way na Andromeda, ni kama wimbo wa mtoto mchanga unaotambulika wakati uko pembeni ya mlango unaounganisha Galaxi zote mbili, wakati mtu anasema mantra tunajiweka moja kwa moja kwenye ukingo huo na ni rahisi “kuruka” tu.
Leo niliingia kutahajudi na niliweza kurudi ukingoni mwa lango na nikachukua “matembezi” kwa kasi kubwa kupitia maeneo ya lengo la manjano na katika safari hiyo nilijifunza kuwa Milkyway ni “binti” wa Andromeda, na kwamba zote zinatafuta kuungana tena kama “mama” na “binti” katika kukumbatia milele.
(M)

 

25 Februari 2021
Nimetokea tu kwa Lengo langu (Dhahabu) na nilikutana na Kiumbe kutoka kwa Galaxy yetu ya Milky Way ambaye alifanya aina hii ya Kusafiri kusaidia Dunia na teknolojia salama maelfu ya miaka iliyopita. Kiumbe huyu alinionyesha uhusiano kati ya Milky Way na Andromeda, na jinsi ambavyo utumiaji wa nguvu ya maisha ambayo pia ni nguvu ya uhai inasababisha kutokuelewana Duniani. Alisema taa zote tunazotumia Duniani sio za asili, na zinavuruga masafa ya usawa ya nguvu ya uhai na kuharakisha mchakato wa kuzeeka wa mwili kufa.

Alinionyesha jinsi wanavyotumia taa zilizowezeshwa kwa kuvuna nguvu ya uhai (nishati ya bure) tofauti kabisa na jinsi tunavyoelewa umeme katika ulimwengu wa kisasa.

Galaxy ya Andromeda ilionekana kama copi na mfano wa Milky Way. Kila kitu kimeunganishwa, kutokuelewana katika hatua yoyote ni kutokuelewana kila mahali.

Kiumbe huyu alihamisha maarifa yake na akasema ni mwanzo wa kuvuna maarifa kwenye mradi ambao tunafanya, kuunda uhusiano kati ya ulimwengu wetu na Galaxy ya Andromeda.
(R)

 
13 Machi 2021
Nilijua Sauti endelevu ya metali na picha iliyoonyejitokeza na kusikika katika ukubwa wa Nafasi. Picha hiyo ilikuwa kama mamilioni ya nukta au duara za kung’aa… angavu sana kati ya nyeupe, dhahabu, na kubadilika taratibu kutoka zambarau hadi kijivu cha metali. … Ilikuwa kama wingu la mapovu madogo? Baadaye niligundua kile nilichokuwa nikisikia kilikuwa ni Sauti ya Galaxy. Picha hiyo ilikuwa sawa na ile ya mamilioni ya nyota ndani ya mkondo mmoja wa mzunguko wa Galaxy.

Katika tahajudi nyingine, nilikuwa nikitazama Nyota, ambayo uso wake ulikuwa kama lava ya dhahabu. Niliiangalia lakini sikuwa na mwili, ilikuwa kama Ufahamu uliopanuliwa. Kutoka kwenye lava hii, moto uliongezeka na moja ya moto huu ulibadilika kuwa Kiumbe na ukawa moto tena kana kwamba unajaribu kuniambia sisi sio tu moto!

Uzoefu huu ni kama ugunduzi wa kibinafsi au kukubalika kwa jinsi nilivyo .. jinsi nisivyo na ukomo… jinsi Kuwa kwangu kunapanuka na kukumbatia Maumbile yote… kuwa Mmoja.
(A)

 

Hitimisho

Inaonekana kwamba Watahajudi wetu waliweza kuungana na malengo mengi na kuona na kuokota habari za kupendeza kutoka kwa Viumbe wanaoishi huko. Tumearifiwa kuwa vikundi vingine vinaendelea kufanya kazi sambamba na sisi na labda pia wamekusanya maarifa ya kushangaza na ufahamu kutoka kwa ziara zao huko Andromeda.