Lugha ya Kiroho

 

Utaona kwamba, wakati unasoma makala kwenye tovuti hii, maneno mengi yaliyotumika huanza na herufi kubwa. Sababu inayotufanya tutumie herufi kubwa ni kwamba lugha ya Kiingereza au Kiswahili hazina misamiati inayoweza kufikisha dhana kuhusu kile ambacho tunaandika. Kisanskriti, kwa upande mwingine, kilichokua na kuendelea katika mazingira ambayo Ufahamu wa Kiroho ulikuwa kawaida kina idadi kubwa ya maneno yanayohusiana na somo hili. Maneno kama vile: Mantra, Atman na Brahman yanapatikana kila mahali kwenye fasihi ya Hindu kama vile Bhagavad Gita.

Kile ambacho tunaweza kufanya ni kuchukua neno la karibu na kutumia herufi kubwa. Kwa mfano: neno upendo, maana yake hisia kali za mapenzi, upendo, huruma nk. Hata hivyo, kile ambacho kwa kawaida tunazungumzia ni uzoefu makali wa jumla na neema ambayo ni zaidi ya ile ya kiakili au kimwili ambayo sisi tunaiita Upendo.

Mfano mwingine itakuwa matumizi ya herufi kubwa katika Uongozi au Utawala. Ufafanuzi wa kamusi wa Utawala unasema: mfumo ambapo wanachama wa shirika au jamii wana nafasi kwa mujibu wa hali zao au mamlaka. Hii inaonyesha kundi la watu wa kimwili ambapo sisi tungekuwa tukimaanisha Viumbe walioko kwenye ulimwengu wa Kiroho ambao tunaweza kutumaini kuwafahamu kidogo kwa ujuzi mdogo kupitia kutahajudi kwetu binafsi.

Ni kosa kubwa kudhani kwamba Ulimwengu hizi za Kiroho ni sawa na ulimwengu wetu wa ‟dimension” tatu au 3-D. Tunafahamu kwamba wakati sisi “tunachunguza” Ngazi za juu, kile ambacho “tunaona” kinapangwa na kuwekwa kwa njia ambayo itakuwa na maana kwetu. Hii pia inaonekana kuwa kweli wakati Wao wanavyo‟tuona” sisi. Hivyo “tunawaona” Wao katika mfumo wa binadamu ambapo Wao wakiwa na Ufahamu wetu sisi tunaonekana kama matone ya mwanga. Tunaweza kuhitimisha kutokana na hili kwamba hivi (Matone ya Mwanga) ndiyo jinsi Wao wanavyofahamiana (dhana).

Matumizi yetu ya herufi kubwa kwa ujumla kutazuiliwa isipokuwa kwa maneno machache vinginevyo maana itapotea na mfumo mzima utakuwa mgumu na kuleta utata. Hatimaye, wakati sisi tunawanukuru Uongozi tutatumia maandishi ya rangi ya magenta.