Kutahajudi Popote

 

Usafari wa London ulinitia moyo kutahajudi katika maeneo ambayo kawaida yasingefikiriwa kuwa mazuri kwa kukaa kimya na kutambua kutoka ndani. Uzoefu unaonyesha kwamba tunaweza kuwa na maswali kuhusu dhana, mawazo na kujenga mabadiliko mazuri.

Sehemu moja ilikuwa kwenye treni, na uzoefu ni kwamba zinaweza kuwa zimejaa wasafiri wanaojisukuma kwenye nafasi yako binafsi, hakuna hewa ya kutosha, joto lililozidi kiasi na hujulikani. Hivyo kwa kawaida sio mahali ambapo ungeweza kuchagua kutangaza “hapo ndipo mimi nitakapo tahajudi!”

Lakini hivyo ndivyo hasa, nilichofanya. Niliamua kuwa itaondoa uzoefu mbaya wa kusafiri na usafiri wa umma wakati wa ‟rush hour”. Kwa mazoezi niliweza kutazama na kuzingatia kwa makini ndani nikiwa mahali popote na wakati wowote. Nilikuwa tayari na nia ya kuchunguza kwa wema na unyenyekevu kwangu mwenyewe na imenisaidia kupumzika na kuzingatia.

Ilisababisha kitu cha ajabu mapema jioni siku moja wakati nachagua kiti kwenye treni. Nilikuwa nimepumzika. Nikafumba macho yangu. Nilijihisi vizuri mwenyewe. Nikaweka mwelekezo wangu ndani. Nikaweka mwelekeo wangu kwenye moyo wangu. Vituo vyangu vya utambulisho au chakra kama ukitaka, vilialianza kutoweka. Haraka, kimoja baada ya kingine. Nilishudia tu vikitoweka.

Alafu nikafahamu kuwa nimekuwa Upendo. Na kwamba Upendo huu uko kila mahali. Upo kwenye kila kitu na unasaidia kila kitu. Hapakuwa na mahali au nafasi ambapo Upendo haukuwepe. Siyo ajabu tu, ni maajabu. Sio maajabu tu lakini ni uzuri halisi. Sasa ninaelewa nadharia inayoelezea kuwa Upendo kama bahari kubwa isiyo na mwisho.

Hivyo tahajudi mahali popote utakapochagua, ili mradi uwe salama. Ni uamuzi wako kwamba ni wakati gani na mahali gani. Ni imani yako ama maadili kuhusu wewe mwenyewe ambayo yatabainisha mahali na wakati wa kutahajudi.