Kutahajudi kwenye Mwanga na Sound

 

Nishati za Mwanga na sauti zimetajwa kwenye vitabu vingi visivyo na idadi na huongelewa na makundi mengi yanayotahajudi. Hata hivyo, kuna aina nyingi za nguvu hizi ambazo ziko kwenye makundi 3 makubwa: kimwili, kufikiri na Kiroho.

Tunataka kuweka wazi kabisa kuwa Nishati tunazozisema hazina uhusiano na ngazi za chini ambazo ni matokeo ya hisia za kimwili na akili zetu. Nishati za Kiroho zinaweza kupatikana tu kwa njia ya nidhamu ya Kutahajudi na Ngazi ya Juu zinahitaji ‟Initiation” ya Kweli ya Kiroho.

Sisi hatutaki kuharibu uzoefu na furaha ya mtu anayegundua Mwanga na Sauti kwa mara ya kwanza. Wala hatutaki kuwapa watu mawazo kwenye akili zao waakaanza kufikiria kuhusu Nishati hizi. Hata hivyo, tunataka tujaribu kuelezea, kwa ubora jinsi tunaweza, kile kidogo ambacho mtu anaweza kutarajia akipata ‟Initiation” ya Kwanza. Kama ilivyoandikwa katika ukurasa wa Safari, hii inafanyika kwa kuguswa kutoka kwa mtu mwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho (Enlightened).

Mwanga na Sauti ambazo zinafunuliwa wakati wa ‟Initiation” zinatoka kwenye Ngazi za Juu zaidi ya mwili na kwa hiyo, kama ilivyoelezwa kabla, hatuzifahamu kwa kutumia akili zetu au hisia. Wakati mwingine imeandikwa katika maandiko kwamba nguvu hizo ni hila. Jambo moja ambalo hizi Nishati sio, ni hila, hata hivyo, mtazamo wa hizi Nishati hutegemea Mtahajudi mwenyewe. Kama umakinifu wao ni kidogo, basi ndiyo, zinaweza kuonekana kuwa hila, lakini kama wanawezi Kutahajudi vizuri, basi ufunuo wake ni wa ajabu kuliko kifani.

Njia bora ya kujaribu kuelewa kile kinachofunuliwa ni kuzingatia kuwa Nishati hizi ni Uhai wenye ‟Akili” ambao unaonyesha Upendo bila Kikimo na Huruma. Nishati Hizi ni Njema kabisa haziwezi kukudhuru wewe. Kinyume chake, utagundua kwamba Zinakuimarisha wewe kwani ndio Asili yako ya Kweli.

Njia hii inakuongoza na kukurudusha Kwako Mwenyewe.

Wakati Mwanga unatazamwa bila chuki, ni mkali kama, “Mwanga wa jua elfu toka angani” (Bhagavad Gita 11:12). Sauti ni ‟orchestra” ya kila chombo cha muziki na sauti za Asili, ambazo zote ziko kwenye Wimbo moja wa ajabu.

Lakini ngoja tena niseme kwamba kile kilichosemwa hapo juu ni kweli tu kwa Mtahajudi anayejitoa hasa, sio mtu ambaye anataka maajabu na uzoefu wa muda mfupi. Kutahajudi Kiroho kunaweza kufanywa na moyo tu – na sio kichwa au akili.

Huwezi kufikiria njia yako kwenda kwa Mungu.

Kwa kweli ni akili, ambayo ni muhimu kwa ajili ya Maisha duniani, ambayo inakuwa kipingamizi cha maendeleo ya Njia ya Kiroho. Si suala la kuisimamisha akili, huwezi, ni suala la kuipita na kiuacha ‟transcendence”. Unahitaji kutafuta njia ya kuzingatia kitu zaidi ya mawazo. Hapa ndipo Nishati ya Kiroho huchukua nafasi muhimu; Zinakupa kitu cha kuweza kuweka mwelekeo wako kukuwezesha kuvuka na kama Zikifuatwa Zitakuchukua wewe na kukurudisha kwenye Chanzo – Asili Yako. Zinaruhusu nafasi ya kuyeyusha Moyo wako, kujifunza jinsi ya “kufa kila siku” (Biblia 1 Wakorintho 15:31).

Hatimaye, Mtafutaji wa Kweli anahitaji kujiandaa iwezekanavyo kwa Kuanziswa ‟Initiation” na kazi yetu ni kuwapa ushauri bora kabisa kusaidia katika maandalizi hayo. Moja ya mtanziko ambao tunakutana nao mara kwa mara, ni lini tutoe ‟Initiation”?

Kwa upande mmoja kama sisi Tukianzisha mapema sana mtu hatakuwa na uwezo wa kupata Nishati vizuri. Kwa hiyo anaweza kukatiswa tamaa na kuacha, na hivyo kuahirisha mwenyewe maendeleo yake ya kiroho na kamwe kuweza kutambua Uwezo wake wa Kweli.

Kwa upande mwingine ni makosa kuwaweka watu, ambao Hutahajudi vizuri, na kusubiri bila sababu yoyote muhimu kabisa. Wao tena wanaweza kupoteza maslahi ya Njia na kuondoka.

Hivyo daima inatubidi tuamue; kitu kikubwa tunachotilia maanani ni kwamba je mtu atafanya nini baada ya Kuanzishwa? Tunataka kuona sifa kama vile uvumilivu, uamuzi, nidhamu na zaidi ya yote..

Juhudi kwa ajili ya Haki na Ukweli.