Ushuhuda (A.O.)

 

Safari yangu ya Ukombozi wa Ufahamu (Enlightenment).

Kulikuwa na safu za tahajudi na za kushangaza kwa siku kadhaa – hali ya utupu, ya kuvutiwa, ya sauti kali sana, kisha sauti na upendo kuunganika; ni kana kwamba sauti ni kila kitu, kila mahali; nafasi ya kina iliyojazwa na sauti na mwanga kana kwamba imeunganishwa na chanzo cha uumbaji na nafasi isiyo na mwisho zaidi ya mwanga.
Kisha mkondo wa sauti unakuchukua kabisa, ni nishati safi, inapanuka haraka sana kupitia mawingu ya mwanga mweupe, hadi kwenye nafasi ya kina kirefu isiyo na mwisho, neema, sauti ya kina, mwanga unaingia ndani yangu.

Mimi ni ufahamu safi, utambuzi safi, ndio hicho tu kilichoko.
Nafasi ya kina isiyo na kikomo na sauti ya kufunika sana, ninainuka na niko huru, niko katika nafasi safi, isiyo na mwisho, isiyo na mipaka, sauti na mwanga huwa moja na mimi ndiyo nguvu hii, upendo unaniingia, mimi ni nafasi, na nafasi imejazwa na upendo, hakuna hisia ya ubinafsi au wakati au mahali, utulivu kamili, uhuru, hali isio na kikomo.

Nimejengwa upya, kama ganda la mayai, vipande vyote vinaenda kana kwamba hakuna umbo lililokuwepo, sipo mahali popote na nipo kila mahali. Nguvu zinaungana kwenye upendo, uzuri, utukufu, mbinguni. Mimi ni roho, kupita kiasi, kufunguka na kufunguka, kupanda mlima kisha kugundua kuwa hakuna mlima, hivi ndivyo nilivyo na ndivyo nilivyokuwa wakati wote – ufahamu safi usio na kipimo au mwisho, kila kitu kila mahali.

Hayo yote yalitokea miezi 6 iliyopita. Na hali hii ya ajabu ya ufahamu usio na mwisho imeendelea kupanuka, kuongezeka, kufunuka, hali ya Uwepo safi, imejaa upendo na uhai na furaha, hali ya ufahamu na kujua ambayo imebadilisha maisha yangu.