Ushuhuda (N.H.)

 

“Wakati nilipokaa kwa tahajudi ya Initiation ya kwanza kweli sikuwa na matarajio makubwa sana. Watu mara nyingi hutia chumvi lakini kwa kawaida ni kwa sababu ya shauku na sio kwa sababu ya udanganyifu. Hivyo nilikuwa hali ya uwazi kiakili ambayo nilikuja kukaa nayo kwenye mto wangu siku hiyo.

Kwa vyovyote nisingeweza kuwa tayari kwa kile kilichotendeka wakati mimi nilipopewa Initiation (Divine Spark); Nilihisi kana kwamba nilikuwa narushwa angani na katika nafasi na kupita galaxies za Mwanga mazuri usiobunika katika rangi nyeupe na dhahabu. Nilichotaka kufanya papo hapo wakati huo ni kufa, kwa kutambua kwamba hata kama mimi nilijichukulia mwenyewe kuwa nimeelimika, sikuwa najua chochote.

Ni wazi niliweza kurudi kutahajudi siku nyingine (niko hai sijakufa). Miaka michache baadaye nikawa Enlightened kutokana na Upendo na Kujitolea kwa mwalimu wangu. Sasa niko kwenye nafasi ya kuwasaidia wengine kwenye Njia ile ile niliyotembea na nitatumia maisha yangu yote duniani kufanya hivyo.

Kufanya kazi na Utawala wa Kiroho kwa Kuwaanzisha watu wengine (kuwa Initiate watu wengine) na kuleta chini Maarifa ni fursa na uwezekano mkubwa ambao mtu anaweza kupewa.”

Post navigation