Enlightenment ndio Lengo la Wanadamu

 


Umeongozwa kuja kwenye tovuti hii – hakuna kinachotokea kwa bahati!

 

Hali ya Kiroho hupatikana kwa kuwa na Ufahamu wa Ulimwengu wa Mbinguni ambao unafafanuliwa katika maandiko mengi kama Mwanga mzuri na Sauti nzuri zaidi ya sauti zote.

 • Nuru inayopofusha na Neno kwenye Biblia ya Kikristo.
 • Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbinguni na Duniani katika Quran.
 • Nuru ya kama Jua mara elfu moja kwenye Bhagavad-Gita.
 •  

  Hali hii haipatikani kwa imani au namna yoyote ya taswira bali kama Ufunuo wa moja kwa moja usiopingika.

  Bila hali za Kiroho watu wanazagaa katika jangwa la kupenda mali. Hawajui walikotoka na hawajui wanakwenda wapi! Uwezekano wa wapi pa kwenda na nini cha kufikiwa katika maisha hauna mwisho, lakini bila nanga ya hali ya Kiroho katika maisha yao wanakuwa wamenaswa kabisa.

  Kihistoria kufahamu kuhusu Nishati hizi za Mwanga na Sauti kulikuwa nadra sana. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni idadi kubwa ya watu duniani kote wamekuwa ‘Wakiamka’ bila kutarajia.
  Hii kwa kawaida ni:

 • Kusikia mchanganyiko wa Sauti za masafa ya juu.
 • Kuona maumbo ya kijiometri au nukta ndogo/miiko ya Mwanga.
 • Kuhisi hisia ya Upanukaji na/au Uwepo wa Upendo.
 •  

  Matukio haya ni kidokezo kwamba kuna zaidi, na zaidi, kuhusu Uwepo wetu. Pia zinatuelekeza kuchunguza!

  Tunawakilisha kundi lisilo na uhusiano wa karibu la Walimu wa Kutahajudi, ambao wengi wao wamepata Enlightenment. Kusudi letu ni kuwasaidia Watahajudi kuwasiliana na kuchunguza Ulimwengu wa Kiroho. Pia tunatoa fursa kwa Watafutaji wa dhati kuwa Walimu ili waweze kuwasaidia wale walio karibu nao kugundua Ukweli.

  Tunachotoa ni cha thamani sana – hivyo kila kitu kinatolewa bure kabisa.

   

  Kuanzishwa

  Kuanzishwa tunakozungumzia ni muunganisho wa kimiujiza ambao hufanywa kati ya Mtafutaji na Ngazi za Kiroho. Hii inafanikishwa kwa “Kugusa” tu na mmoja wa Walimu wetu. Mwalimu ni mtu ambaye amefuata Njia ya Mwanga na Sauti na kupata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Muunganisho huu ni wa kudumu lakini unahitaji mazoezi ya mara kwa mara ya Kutahajudi ili kuongeza na kukuza faida yake.

  Nguvu hizi za Mungu zipo kukuongoza kwenye Njia ya Kiroho na Kukufundisha mafunzo unayohitaji kujifunza. Ufunuo wa kuvutia wa Ajabu, zaidi ya mawazo yote, hufunuliwa na mwishowe zinaweza kukupeleka kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.

   

  Uamsho

  Nishati ya Kiroho kwenye Sayari hii iko katika kiwango cha juu sana kwa wakati huu. Hii inamaanisha kwamba idadi kubwa ya watu kote ulimwenguni wanapata Uamsho wa kushangaza bila kutegemea, wengine wanapata hata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Mara nyingi Uzoefu huu ni wa ajabu sana hivi kwamba watu wanakuwa na mashaka kuwa ni halisi. Tunafurahi wakati wowote kutoa ushauri, ambao kwa mara nyingine tena, ni bure kabisa, na kutoa wasiwasi wowote. Tunaona Uamsho huu kama kidokezo cha kitu kikubwa… Njia ya Kiroho inayofikia mwisho katika Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.

  Tunayo tovuti nyingine ambayo inazingatia Uamsho na Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Ina Ushuhuda wa kushangaza, mwingi kutoka kwa watu ambao hawajawahi hata kutahajudi.


  www.awakeningenlightenment.com

   


   

  Ukombozi Wa Ufahamu au Enlightenment

  Neno hili limetumika katika enzi zote na hubeba wigo mzima wa maana. Kwa hivyo ni muhimu kuelezea haswa kile tunachomaanisha kwa Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Kwa hivyo tumechukua ukurasa mzima wa tovuti hii kuifafanua, na kuweka ushuhuda wa watu ambao tumewasaidia kupata Hali hii.

  Kwa sasa tutasema tu kwamba Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au Enlightenment ya kweli ya Kiroho hufanyika wakati mtu anapoungana na Umoja na kupoteza kabisa ubinafsi wake au kile anachojua na yeye.

   

  Uongozi Wa Kiroho

  Mnamo Februari mwaka 2015 idadi ndogo ya Watahajudi ambao walikuwa wapepata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment walipata mawasiliano na Uongozi wa Kiroho. Viumbe hawa wametokea mara nyingi huko nyuma. Wakati mwingine kwa watu binafsi na wakati mwingine kwa vikundi kama vile Theosophical Society ambao walitunga jina, Uongozi wa Kiroho au Spiritual Hierarchy.

  Kusudi kawaida ni kusaidia kumwongoza mtu binafsi, au kutoa maarifa kusaidia binadamu. Nguvu za Kiroho zinafunuliwa kwa watu wa Sayari hii kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tena! Tunauita muujiza huu kwa jina la Lightwave Mpya.

  Tunayo tovuti nyingine ambayo imewekwa maalum kwa ajili ya Uongozi Wa Kiroho. Ina Ujumbe mwingi toka kwao ambao unavutia kusoma.


  swahili.spiritualhierarchy.com

   

  Dunia Nzima

  Ukurasa wa “Dunia Nzima” una mwaliko wa wazi kwa Watahajudi, kote Duniani, kuungana nasi katika kutuma Upendo na Mwanga kwenye Sayari yetu ya thamani. Ni muhimu sana kuamka na kushughulikia maswala ambayo yanatishia idadi kubwa ya viumbe na mimea ambyo inaishi kwenye Dunia yetu hii nzuri. Tunahitaji sana kurejesha usawa na uelewano haraka iwezekanavyo.
   

  Msukumo

  Watu ambao wanatafuta Ukweli mara nyingi wanahitaji uhakikisho kuwa kuna wengine ambao wana Jitihada sawa. Watu wengi wanatembea kwenye Njia ya Kiroho, lakini inaweza kuwa na upweke kwani lazima Utembee peke yako. Ni muhimu kuzingatia na nidhamu kudumishwa ikiwa mtu anataka kufikia Lengo lake.

  Kwa hivyo tunatoa makala kadhaa za kusaidia kukuza na kumhamasisha mtu kwenye Njia ya Kiroho. Ufahamu wa Kiroho au Enlightenment haipatikani kamwe kwa maneno lakini maneno ni muhimu sana kumwelekeza mtu kuelekea kwenye mwelekeo sahihi.

   

  Ushuhuda

  Ikiwa unaanza safari unataka kujua kuwa njia uliyochagua itakuongoza na kukufikisha mwisho wa Safari yako. Cha kushangaza, ikiwa unafuta Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment huwezi kujua Mwisho wa Safari kabla hujafika. Unaweza kusoma maelezo lakini unahitaji kuamini (trust) kuwa hiki ndicho haswa Unachotafuta!

  Kwa hivyo tumekusanya Ushuhuda mbali mbali kutoka kwa watu waliopata Uamsho bila kutegemea na/au wametahajudi kwenye Nguvu za Mwanga na Sauti. Tumejumuisha pia Ujumbe mchache kutoka kwa watu waliopata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment na Walioacha maisha yao ya Duniani na Kupanda kwenda kwenye Ngazi za Kiroho.

   

  Ukurasa Wa Mawasiliano

  Tumetoa ukurasa wa mawasiliano ili uweze kuwauliza Walimu wetu maswali yoyote yanayohusiana na Elimu ya Kiroho na Kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya Mungu.
  Wasiliana na Walimu wa Kutahajudi

   

  Tunapenda kumshukuru Amanda Sage kwa huruma na ruhusa yake ya kutumia picha nzuri ya Limbic Resonance inayoonyesha Uhamisho wa Nishati ya Kiroho kati ya wanadamu. www.amandasage.com