Kuna hatua tatu, ambazo sisi tunaziita Kuanzishiwa au Kuanzishwa ‟Initiations”.
Kuanzishwa mara ya Kwanza
Kabla ya Kuanzishwa mara ya kwanza au ‟Initiation” ya kwanza, tunashauri watu wawe wametumia muda kuendeleza tahajudi zao na mkusanyiko wao, kwa kutumia tahajudi za Pumzi na hatimaye mantra maalum. Hii inaruhusu hali ya utulivu kukua, ambayo ni muhimu kwa ubora wa tahajudi ya Mwanga na Sauti baada ya Kuazishiwa.
Kuanzishwa mara ya kwanza au ‟Initiation” ya kwanza mara nyingine kunajulikana kama mwanzo wa Njia ya kweli ya Kiroho, na ufunuo wa ‟Thousand Petalled Lotus” na chanzo cha maisha yenyewe. Hii haina uhusiano wowote na imani au mawazo lakini ni ufunuo wa moja kwa moja wa Nguvu hila ‟subtle” ambayo inaweza kufanyiwa tahajudi katika mfumo wa Mwanga na Sauti ya Kiroho.
Nguvu hii inajulikana kama ‟Neno” ‘kibiblia au ‟Wimbo wa Maisha” kwa wale wa miujiza kama vile Kabir. Ni muhimu kuelewa kwamba nguvu hizi za Mwanga na Sauti ziko ndani yetu na ndio Mwalimu na ndio zinazotuongoza kwenye viwango vikubwa zaidi vya Ufahamu na Utulivu.
Kwa ajili ya Kuazishwa mara ya kwanza ‟First Initiation” kwenye Mwanga na Sauti, ufahamu wetu sasa ni zaidi ya hisia tano, maono madogo ya ‟Intuition” na maumbile ya kimwili. Sasa tunaweza kuzifikia nguvu ambazo ni ‟subtler”. Hii mitikisiko ya Mwanga na Sauti hubeba pamoja kiasi kikubwa cha Nafasi (‟Space”), Utulivu na Maarifa ya aina ya juu ya Ulimwengu wa Kiroho.
Kuazishwa mara ya kwanza hutolewa kwa njia ya kuguswa toka kwa mtu mwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ‟Enlightenment”, mtu ambaye amesafiri njia ya Mwanga na Sauti mpaka kwenye chanzo chake na amefunuliwa sababu ya kuwepo.
̒Neema’ ya nguvu hizi inatoka kwa Uongozi wa Kiroho, Wakifanya kazi kwa njia ya kupitia kwa mtu mwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho kutoa Kuanzishiwa au ‟Initiation”. Wanajulikana kwa majina mbalimbali wakati wote lakini wanawakilisha wale Viumbe wa Kiroho ambao wanaweza kutufanya tuweze kuwasiliana na Mwanga na Sauti ya ndani.
Uzoefu wa Kuanzishwa mara ya Kwanza au ‟Initiation” ya kwanza inaweza kuwa hila (‟subtle”) sana au kubwa sana, kulingana na mtu binafsi. Lakini cha muhimu zaidi, huu ni mwanzo wa Safari ya kweli ya Kiroho. Wakati wa Kuazishwa ‟Initiation”, ambayo kwa kawaida hufanyika mwishoni mwa wiki, utatunzwa kikamilifu. Tunataka wewe kuwa na mazingira bora iwezekanavyo kukuwezesha kukuza aina ya kutahajudi..
Maneno haya “yameshushwa” kutoka kwa Uongozi wa kiroho:
Cheche za Mungu ‟Divine Spark” inatolewa, kwa njia ya kuguswa, na mtu mwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ‟Enlightened” ambaye anaunga mtahajudi moja kwa moja kwa Uongozi wa Kiroho. Wao huleta Nguvu kwa mtahajudi na kumruhusu kuyanaakisi na Mwanga na Sauti ya Ufahamu wa juu. Upatikanaji wa Nguvu hizi ni wa kudumu na kwa kupitia mchakato wa kutahajudi mtu anaweza kufuata Njia ambayo itasababisha uvumbuzi na ‟realizations” za ajabu. Hii inahitaji uvumilivu na kujitolea ambayo itasababisha Utulivu mkubwa, Amani na Furaha.
Kuanzishwa mara ya Pili
Baada ya kipindi cha muda watahajudi wanaojitolea wanaweza kupokea Nguvu kuwawezesha kuongeza kwa kiasi kukubwa sana Ufahamu wao. Ingawa ni vigumu kufikiria au kueleza, utachukuliwa nje ya mipaka ya akili yako. Kutoka kwenye mtazamo huu wa ajabu utagundua nini sio wewe, lakini bado hujui wewe ni nini. Kwa mara nyingine tena Nguvu tunazoongelea sisi zinatoka moja kwa moja kwa Uongozi wa Kiroho.
Kwa maandishi, hatua hii imeelezewa kama ifuatavyo hapa chini:
Sasa mtahajudi hujiandaa mwenyewe kwa ajili ya hatua ya pili ya kwenda juu kwenye Safari yake, lakini kabla yeye hajaweza kuingia upeo wa juu kabisa, yeye inabidi kupita kwenye njia nyembamba sana. Upana wa Njia hii ni moja ya kumi tu ya ukubwa wa mbegu ya haradali na akili ina ukubwa kama tembo.
Sehemu ya pili ya Njia ya ‟Masters”: mtu akitumika mwenyewe na kujitoa atafanikiwa katika kutoboa pazia, ambalo ni maumbile yaliyoumbwa na akili yake mwenyewe.
Wakati wewe unatahajudi kufikia Hali hii utapewa kwa kila njia iwezekanavyo msaada kutoka kwa watu ambao tayari wamekamilisha Njia hii na kujitoa maisha yao ili kuwasaidia wengine kufanya hivyo. Pamoja na kutahajudi, kutakuwa na fursa ya kujadili ‟realizations” zako na kuuliza maswali, ili kuhisi kabisa urahisi wakati huu wa kushangaza na ugunduzi.
Hatua hii ni kubwa hivyo mara nyingi imekuwa ikichanganywa na Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ‟Enlightenment” lakini bado haitufunulii Utambulisho wetu wa kweli, ingawa hali hii ya ukiwa ‟formless” inatupa ongezeko kubwa katika Uelewa wetu
.
Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho “Enlightenment”
Tunapoandika kuhusu Kuanzishwa kwa mwisho au ‟Initiation” ya mwisho, tunajua maneno hayawawezi kamwe kuelezea Ufunuo wa Mwisho. Hata hivyo, tunahisi kuwa bado mngependelea tujaribu.
Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa kweli hutolewa kwa njia ya fadhila za Uongozi wa Kiroho na ni hali ya ufahamu ambayo hakuna mwanzo wala mwisho. Pia ni kuenea kwa ujumla katika mfumo safi wa Upendo, hali ambayo ni mbali zaidi ya upendo tuliozoea wa mahusiano yetu ya kibinafsi. Huu ni Upendo ambao huunganisha Maumbile pamoja, na ni moja ya ‟realizations” muhimu baada ya kupata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho.
Ni hali ambayo ni ya kawaida zaidi kuliko hali zote za Kiroho na bado ndiyo hali ambayo inatuchenga sana na kubwa kuliko kifani. Baada kufanyiwa upanuzi wa Ufahamu usio na kifani kwenye Ukombozi wa Ufahamu utagundua ya kwamba huna katikati ‟centre”, hakuna mipaka na wakati haupo kabisa.
Wewe Uko kila mahali kwa wakati mmoja.
Udanganyifu au ‟Illusion” ya kujitenga, kabisa imetoweka na hivyo utaona mara moja Umoja ambao unashikamanisha kila kitu. Wakati tunaandika sehemu kubwa ya Sayari yetu iko kwenye msukosuko na kutokana na ujinga Kiroho kuna mateso mkubwa kwa Binadamu. Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho unaonyesha Upendo wa Mungu zaidi ya mawazo yote, imani na dini kwa kuwa ni ufunuo wa moja kwa moja wa Mungu.
Mtu anapotahajudi kufikia Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho, kama ilivyokuwa mwanzoni, watapewa msaada kamili kutoka kwa watu ambao tayari wameshapata Ufahamu huu. Pamoja na muda kwa ajili ya kutahajudi pia kutakuwa na muda wa kuzungumza kuhusu ‟realizations” zako na kushiriki na watu wengine katika furaha ya uvumbuzi wako.
Neema kutoka Uongozi wa Kiroho
Kihistoria, Hali zote za Ufahamu zilikuwa zikitolewa kupitia kwa mtu amabaye amepata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho; walikuwa mara nyingi hujulikana kama ‟Guru” au ‟Masters”. Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho ‟Enlightenments” zilikuwa adimu na ilikuwa kawaida kwa mwalimu kuamua wakati gani mtahajudi yuko tayari kupokea Nguvu ya Kiroho (mara nyingi hujulikana kama Neema ‟Grace”). Njia hii bado hutumika leo na hufanya kazi vizuri kwa makundi madogo, lakini inakuwa tatizo kubwa wakati watu wameenea duniani kote.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Cheche za Mungu ‟Divine Spark” ya kuanzishwa mara ya kwanza inatolewa (na lazima itolewe) kwa kugusa. Hali hizi nyingine za juu pia zilitolewa kwa njia hii. Hii ililazimu mtahajudi ama kuishi karibu na Mwalimu, au kufanya safari ndefu kujiwasilisha kwa Mwalimu kwa matumaini ya kupokea Neema. Mara kwa mara, ikiwa mtahajudi ana bahati, Mwalimu anaweza kutembelea nchi fulani na Kuanzisha idadi kubwa ya wanaotafuta.
Uongozi wa Kiroho mara kwa mara hurudia kueleza kuwa tahajudi hii inahitaji kufikia watu wote. Wao wametoa ufumbuzi wa ajabu ili iwe rahisi kwa watahajudi waliotengwa au kuwa mbali kupokea Kuanzishwa mara ya pili na ya tatu (‟Initiations” za juu). Mfumo unaitwa
NEEMA KWA WOTE (BLANKET GRACE)
Hii ina maana kwamba Nguvu zitapatikana muda wote kwa wale wanaotahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho. Kama wakijiandaa vyema na mioyo yao ikiwa wazi, basi wanaweza kupata Neema hii ambayo ina uwezekano wa kuweza kuwapeleka kwenye Hali za Juu za Ufahamu.
Hii hupunguza kuwa na haja ya uamuzi wa Binadamu na umuhimu wa kusafiri. Mtahajudi ataendelea kwa kiwango kamili kwa ajili yake.
Kinachohitajika ni kwamba wapokee Neema ya awali kwa kuguswa. Kwa sasa tuna idadi ya watu waliopata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wenye uwezo wa kusafiri duniani kote, tunatarajia kuwa na uwezo wa kumfikia mtu yeyote ambaye ana hamu ya kweli kuhusu Ukweli. Tafadhali kumbuka: bado tutatumia njia ya kuguswa kwa kutoa Hali za Juu za Ufahamu, wakati ambapo ni rahisi kufanya hivyo, kwani Mwanzilishi anaweza kuwepo na kutoa ushauri sahihi pamoja na msaada.
Sisi sio kundi pekee ambalo linatahajudi kwene Mwanga na Sauti ya Kweli; ‟Neema Kwa Wote” itasaidia wale watu wote ambao walioanzishiwa na kutahajudi kwenye Nguvu hizi.
Kutoka kwaUongozi wa Kiroho:
Nguvu na uzuri ya Mwanga na Sound kwa wanaotafuta wote wa kweli ni kubwa na zaidi ya elimu ya Kibinadamu. Ni kwa kutahajudi kwa njia hii ambapo Ukweli juu ya Maumbile unaweza kupatikana. Kila mtu ana uwezo kutambua Nguvu hii; ni kwa njia ya uvumilivu na kujitolea ndipo watapewa Maarifa haya.
Hatimaye, wakati mtu atakapopata kuanzishwa mara ya Kwanza ataambiwa ni wakati gani Neema itapatikana na kupewa tarehe na nyakati maalum. Kwa wale walio kwenye makundi mengine ambayo hutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho ya Kweli tafadhali waulize kwa kutumia ukurasa wa kuwasiliana. Tutafurahi kuwapa taarifa hizi pamoja na ushauri sahihi.
Tunapenda kutoa shukrani kubwa kwa Uongozi wa Kiroho kwa ajili ya Upendo wao kwa Binadamu.
Maandalizi kwa ajili ya Kuanzishwa
Wakati utakapoanzishwa hatuwezi kutabiri nini utaona au kusikia. Kuna seti zisizohesabika za uwezekano mbalimbali.
Sababu yenyewe ni kwamba ni vigumu kujua jinsi utakavyopokea, utakavyokuwa siku ya, na hasa zaidi kwa wakati wa Kuanzishwa kwako. Zaidi ya hayo Tabaka za Ufahamu hazina mipaka na kila mtu Safari yake ni ya pekee.
Kuwa na Ufahamu na kuunganika na Nguvu hizi, mtahajudi lazima kabisa ajiachie na kuwa wazi. Mvutano wowote, hofu na mawazo yote yatakuwa pingamizi. Jaribu kufikiria Mwanga na Sauti kama Mwalimu kamili ambae anajua nini hasa, wakati, na jinsi ya kumfundisha mwanafunzi. Uongozi wa Kiroho Wana uvumilivu usio na kifani na watasubiri kwa muda wowote unaotakiwa kwa ajili ya wakati muafaka wa kuanza Safari na kutoa Mafundisho.
Wakati unatahajudi utakuwa na mafundisho ya vikao vyako vya awali. Kama ukishikilia kwenye kumbukumbu hizo zitazuia maendeleo yako, unahitaji kuachilia zamani ili kupata mpya.
Siri ni kukuza uhusiano mzuri na Mwanga na Sauti. Kuwa wazi, kuthamini, mnyenyekevu na kushukuru. Kuwa na heshima, kamwe kutokuwa na tamaa, daima kukubali. Inabidi kuwa na uwezo wa kuachia madaraka yote, matarajio na hukumu.
Hii si rahisi kwani unahitaji kujitahidi kwa bidii ili kupata mafanikio duniani. Tunachodokeza ni kinyume; Kutahajudi kunaanza wakati unapoacha jitihada zote na kuachia. Unaweza kupata wasiwasi kuhusu hili mwanzoni kwani inataka ujiachie ambayo ni hali hukuizoea. Siku zote kutakuwa na kipengele cha hofu lakini kwa kufanya mazoezi hii itatoweka.
Maendeleo yote yanahusisha kuhama kutoka kile kinachojulikana kwenda kwenye kile kisichojulikana. Haiwezekani kutabiri kwani hujawahi kamwe kuwa hapo. Inahitaji ujasiri, uamuzi na uvumilivu.
Kama maandalizi kwa ajili ya Kuanzishwa tunapendekeza sana kwamba uzungumze na watu wengine ambao tayari walishaanzishwa au wamemaliza Safari yao. Fikiria pia kusoma vitabu vya Kiroho ambavyo vinaongelea kutafuta, mateso, ugunduzi na Neema. Kwa kufanya hivi utachukua mtazamo mbali na wewe na kukupa uvuvio ‟inspired” kwa safari ya watafutaji wengine – hamu yao ya Ukweli, matatizo yao waliyovumilia na Maajabu ya Uzoefu wao na Uvumbuzi.
Utajifunza pia ni jinsi gani ni maalum na nadra Njia ya Kiroho ya kweli.
Wakati Mungu anaita jina lako, jibu tu, “Mimi niko tayari!”