Sauti Ya Kiroho

 

 

Watu Wanasikia Sauti ya juu

 
Tunatambua kuwa idadi kubwa ya watu (wengi ni vijana) wamekuwa na ufahamu wa sauti ya juu ambayo haionekani kuwa asili ya kimwili.

Maelezo yao wote ni sawa kabisa, wanasikia sauti ya juu mara nyingi ikiwa na nguvu isiyobadilika “steady”. Wanaweza kusikia sauti hii hata wakiwa kwenye mazingira yenye kelele lakini kwa kawaida hutokea wakati mtu akiwa ametulia, na mara nyingi kabla ya kwenda usingizini.

Kama ukitaja kwa watu, wengi wao wanasema kuwa hawajapata kusikia sauti hiyo. Hata hivyo, cha kushangaza ni kuwa wachache wanasema: “Ndio!, au ghafla inatokea wanaisikia Sauti”. Hawakuwa na ufahamu wa Sauti hii mpaka tulipo waambia. Ni kana kwamba tunaweza kwa namna fulani kuwa “tune”! Mara baada ya kusikia, wao wanaendelea kuwa na uwezo wa kuipata na kusikia Sauti.

Tumeambiwa kuwa sababu ya Sauti kusikika ni kwa sababu ya Kuanzishwa(“initiations”) na Ukombozi wa Ufahamu (“Enlightenments”) ambazo zinafanyika na kutokea kote Duniani. Kiasi cha Nishati ya Kiroho ambayo inaelekezwa Duniani ni kubwa sana haijawahi kutokea nyakati za karibuni.

Sauti hii ipo daima lakini watu hawawezi kusikia mpaka wapate msukumo “activation” wa “Lightwave”. Ni sawa na “kiitikio cha alfajiri”; wakati mionzi ya kwanza ya jua inapoanza kuchomoza angani, ndege huanza kuimba na “Nature” inaamshwa toka “usingizini”.

Inaonekana kwamba binadamu na dunia sio tofauti na tunategemeana. Maslahi yetu kimwili na Kiroho hutegemea hali ya Sayari yetu. Kwa miaka mingi sisi tumekuwa tunapora na kufuja rasilimali za madini na kuharibu maisha ya viumbe vingi kwa kuharibu mazingara na makazi yao. Ingawa sisi hatujui, ugonjwa wa Sayari imekuwa na athari mbaya kwa Binadamu. Tumekuwa na uchoyo wa vitu na tumesahau kuwa na huruma kwa Wanadamu wenzetu. Maadili na harakati za kutafuta elimu ya Kiroho imechukua nafasi ya mwisho kwenye jamii ya “mimi kwanza”.

Hii ndiyo sababu ya kuanzisha “Njia”, kuleta elimu ya Kiroho kwa watu wote. Hii sasa imesababisha mwamko wa kiinishati wa Sayari; ni kana kwamba inaanza “kuimba”. Hapo awali, mtu angehitajika kupata “Initiation” ili kuweza kusikia Sauti hii lakini sasa idadi ya watu wanaoisikia inaongezeka.

Uliza familia yako, majirani na marafiki kama wanawezi kuisikia. Unaweza kushangaa jinsi ambavyo hii ni kawaida. Wengi watakuwa na mshauko, ikiwa hivyo, tafadhali waelekeze kwenye tovuti hii ili kuwasaidia kuelewa Ukweli juu ya hicho walichokisikia.

Tafadhali tujulishe ulichosikia; tungependa kujua jinsi ambavyo hali hii imeenea na jinsi watu wanavyosema.

 

Ushauri Wa Kutahajudi kwenye Sauti

 
Kama unasikia Sauti za juu tunapendekeza sana kwamba ujifunze kutahajudi kwenye Sauti Hizi. Ulichopewa ni zawadi ya ajabu ambayo kama ikitumika kwa uwezo wake kamili itaonyesha ufahamu mkubwa wa asili yako ya kweli ya Kiroho.

Unaweza kuwa umesoma kwamba wahenga wakubwa na MaYogi katika nyakati zote wametumia Kutahajudi kama chombo cha kufungua Siri na kugundua Hali za furaha na ajabu pamoja na Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho yaani Spiritual Enlightenment. Wao pia walikuwa na ufahamu wa mkondo huu wa Sauti na waliitumia kulengo ndani kwenye Tahajudi zao.

Mkondo huu wa Sauti huelekea kuja na koundoka kana kwamba una akili yake yenyewe. Jaribu kutafuta mahali fulani pazuri pa kukaa; hii inaweza kuwa juu ya mto au kwenye kiti. Ni vyema kuweka mgongo wako ukiwa sawa na umenyooka kuelekea juu. Weka mtazamo wako kwa upole kwenye Sauti bila kujaribu kuichambua kiakili; iache iwepo tu!

Unaweza kuhisi au kuona kuwa inapata nguvu na kuongezeka na itakuwa na kina zaidi. Kadiri unavyozidi kujifunza kupumzika na kujiachia Sauti itaonekana kama kupanuka kwa kile ambacho unahisi ni Wewe. Kadiri unavyozidi kujifunza ku tiuni ndivyo zaidi Sauti itakuwepo.

Huenda ikawa kwamba Sauti itatokea na kusikika wakati unatembea nje. Ili mradi huna haja ya kupita barabara yenye magari au njia yenye hatari unaweza kutahajudi wakati unatembea. Unahitaji tu kuunganisha Sauti pamoja na hisia zako zingine za (kimwili). Hii sio ngumu kama inavyoonekana kwa kufanya mazoezi kidogo itakuwa ni namna ya kawaida ya kuwa. Utakuwa na uwezo wa kuishi katika dunia na zaidi ya Dunia kwa wakati mmoja. Kuwa na ufahamu wako wa kimwili na Ufahamu wako wa Kiroho kwa wakati huo huo hakika ni njia ya kawaida ya kuwa!

Zaidi ya hayo, unaweza kuona kwamba unaanza kuona mwanga unapofunga macho yako. Sisi hatumaanishi mwanga wa akili lakini Mwanga wa Kiroho. Hii itachukua muundo wa maumbo na rangi ambazo zitakua na kuwa wazi na kali kadiri unavyojifunza Kutahajudi zaidi. Kama kwenye tahajudi ya Sauti, jaribu kutochambua na kutochanganua kile unachokiona. Angalia tu bila kuchanganua au kupendelea na acha Mwanga uwe tu.

Mara utakapojaribu kuingiliana na Mwanga utatoweka. Jiachie na kuwa macho tu na uruhusu Siri ifunuliwe kiasili. Nguvu ya Mwanga na Sauti itakuchukua wewe kwenye Safari ya ajabu ambayo kuna uwezekano wa kuishia kwenye Ukombozi Wa Ufahamu wa Kiroho ni Enlightenment ya Kiroho!

Huenda ikawa unahitaji msaada. Kwa hali yoyote ile omba msaada kwa mmoja wa Watahajudi wetu ambao tayari wametembea Njia hii ya Kiroho. Wana uwezo wa kuhamisha na kukuongezea Nguvu na kuifanya Safari yako ya Kiroho kuwa rahisi zaidi.