Kwa kawaida watu ambao wanataamuli kuwa na Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho walizingatia seti ya sheria kali kuhusu maisha. Hizi ni pamoja na ulaji mboga, kuacha pombe na madawa ya kulevya; na mara nyingi useja kabisa ulihitajika. Lengo letu ni kufanya Safari hii ipatikane kwa watu wote kwa wakati huu kwani hali ya dunia yetu iko hatarini na kuna haja kubwa ya kuleta nguvu nyingi ya Kiroho.
Tukiwa nalo hili akilini tunahitaji kulegeza zaidi na kutumia busara kwa kile ambacho tunataka mtafutaji afanye. Sisi tunachopendekeza ni kuangalia mambo yote kwa busara na kuwa na kanuni ya kuwa na kipimo. Sababu ya vikwazo kuwekwa hapo mwanzo ilikuwa kumfanya mtahajudi apate nafasi nzuri ya kuwasiliana na Nguvu za Kiroho. Hivyo kama tahajudi yako sio rahisi basi uwe na hekima ya kuzingatia na kuangalia jinsi unavyoutunza mwili wako.
Jambo la muhimu pia ni kiasi chako cha shinikizo na unahitaji kushughulikia masuala ya kujitolea na usimamizi wa wakati kama wewe utafikia lengo lako la Kiroho. Awali tunakwambia kuwa ujenge uwezo wa kutahajudi kwa muda wa saa moja kila siku lakini ili kufikia ufahamu wa hali ya juu, watatakiwa kuweza kutahajudi kwa muda mrefu zaidi siku zijazo. Baada ya kusema hivyo, ni ubora wa kutahajudi ndiyo muhimu si lazima uwingi.
Baada ya kupokea Cheche za Mungu “Divine Spark” na ku“resonate” na Mwanga na Sound utajifunza haraka kwamba huwezi kudhibiti Nguvu hizi. Zitaonekana tu wakati unakuwa wazi kabisa na zitakushangaza. Kwa hiyo tunapendekeza mazoezi ya vitendo vya hisani ili kutengeneza “nafasi ndani”, ili kufanya iwe rahisi zaidi wewe kuweza kupokea wakati wa kutahajudi
.
“Kila kitu kina ufa ndani yake, hivyo ndivyo Mwanga unavyoingia ndani.” (Leonard Cohen)
Mazoezi
Ingawa wanaotahajudi wanafanya mafunzo ya kuwa wapiganaji wa Kiroho na sio wanariadha, kiasi fulani cha mazoezi sio vibaya. Tunapendekeza shughuli za upole zaidi za kutembea, kuendesha baiskeli, kuogelea na yoga. Utaratibu wa mitiririko ni vyema na utumiaji wa nguvu kwa muda mfupi wakati wa mazoezi unaweza kuzingatiwa. Usisahau kwamba mara nyingi unaweza kuchanganya mazoezi na kutumbelea asili “Mother Nature: hii huongeza uzoefu mzima na kubadili jukumu kuwa jambo la kufurahia ambalo utataka kulirudia.
“Vegetarianism”
Tungependa sana kupendekeza kwamba unajitahidi kuelekea kwennye vyakula vya mboga mboga (hakuna nyama, samaki au mayai) lakini ikiwa ni pamoja na bidhaa za maziwa. Ukitaka kufanya hivyo, fanya mabadiliko hatua kwa hatua kwa kipindi cha muda wa miezi kadhaa, vinginevyo unaweza kuwa na mshtuko mkubwa kwa mwili wako; Tunajua jambo hilo kwani binafsi tumeyapitia hayo yote! Unavyozidi kutahajudi utakuwa makini zaidi na utaweza kufanya mwenyewe uchaguzi wa mboga kama kawaida. Hii ni njia kamili ya kuangalia swala hili:- “Sikiliza mwili wako mwenyewe.”
Kisayansi imeonyeshwa kuwa mwili wa binadamu unaweza kuvunjavunja vyakula vya asili ya mimea kwa kasi cha mara 3 zaidi kuliko vyakula toka kwenye nyama. Pia utafiti inaonyesha kwamba walaji mboga huwa na kuwa na afya njema na kwa sababu hiyo wanaishi, kwa kawaida miaka 5 zaidi kuliko wengine. Hata hivyo, sio maisha marefu ambayo yanatufanya tupendekeze hii, lakini hii ni kukusaidia kuweza kutuliza mwili ili uweze kuwa na ufahamu zaidi na undani wa maajabu ya ndani kwenye tahajudi yako.
Pombe
Pombe huathiri watu mbalimbali kwa njia tofauti na pia inategemea na kiasi. Wakati wa kukaa na kutahajudi ni muhimu kwamba unaweza kuzingatia kabisa na mtazamo wako na kuwa wazi kabisa. Kama umekunywa pombe kiasi kikubwa utaona kuwa hii haiwezekani kabisa na itakuwa inavuruga maono yako. Kwa hiyo hatupendekeza unywaji pombe kiasi kikubwa hasa kama unataka kufikia ufahamu wa juu.
Kuna vinyaji vingi ambavyo havina kileo au pombe na vingine vyenye kiasi kidogo cha pombe kwenye soko sasa hivi kwa hiyo bado unaweza kuwa na maisha ya kijamii na kufurahia faida ya ajabu ya kutahajudi kwa wakati mmoja. La kufanya ni kuwa na kiasi!
Madawa
Ni madawa ya kulevya ambayo tunaongelea hapa na sio dawa ulizoandikiwa na daktari wako / mfamasia, kwa madhumuni ya kukutibu. Dawa hizi kwa ufafanuzi, daima zitabadilisha hali yako ya fahamu kupitia michakato ya biologia na kemikali. Hii inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kimwili, kihisia na kiakili na kwa muda mfupi itakuwa pingamizi ya uwezo wako wa kutahajudi vizuri.
Kwa hiyo tunaushauri sana kutafuta kupanua ufahamu na hali yako na hali hizi kwa kutumia njia salama, ya upole na asili ya mchakato wa kutahajudi. Hebu fikiri jinsi ambavyo mayogi wakubwa walivyojifanyia katika kujaribu kusafisha miili yao: – Hapa tena tunasema kwamba wewe tumia akili yako!
Ni muhimu kwamba usijisikie kuwa una hatia kuhusu maisha yako, lakini kuwa na malengo ambayo ni ya busara na ambayo yanawezekana kufikiwa, na unaweza kufanya kazi kwa upole kuelekea kwenye lengo lako kwa kadiri ya uwezo wako mwenyewe. Tunapendekeza kwamba uzungumze na watahajudi wengine kwani uzoefu wao binafsi unaweza kukusaidia kufanya maamuzi ya hekima kuhusu mabadiliko yoyote unayojisikia na kutaka kufanya. Pia jisikie huru kuuliza kwetu maswali yoyote maalum kuhusu mada hizi: tutafanya kila tuwezalo kujibu na kuyaweka majibu kwenye ukurasa wa “Maswali na Majibu”.
Kutoa
Safari zote za kiroho ni matokeo ya Kutoa kwa dhati kutoka kwa Utawala wa kiroho: Hawahitaji kitu chochote. Tunataka kuiga ukarimu wao kwa kutumia mfumo wa kuruhusu watu kuonyesha kutoa kwa fadhili na huduma wakati wa kushughulikia watu wengine.
Kushawishika kwetu kulitokana na kanuni iliyotoka kwenye kitabu / filamu “Lipa ni Forward”. Ingawa ndoto, inaweza kuwa kama “Tenet” ya msingi ambayo Ufahamu wa Kiroho utawafikia watu wote. Inasema kwamba badala ya kumlipa mtu aliyekufanyia jambo zuri wewe utalipa mbele kama mara tatu. hii hutoa fursa za kuwajali wengine, kueneza Ukweli na Kuzuia mitego mingi inayohusiana na fedha.
Hivyo tunasema kwenu wote, yote yanayofanywa ili kukusaidia katika safari yako ya Kiroho ni BURE kabisa kwa maana ya fedha na BURE kwamaana ya majukumu na madeni yote. Hata hivyo, kama wewe kwa upande wako unataka kusaidia au kulea mtu kuelekea lengo moja kama lako tunawasihi kukumbatia kanuni hiyo na kutoa BURE kwa mtu au watu wengine.
Kama kila mmoja wetu atalea watu wengine WATATU na kupata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho na wale WATATU wakafanya hivyo, baada ya hatua 21 tu tungeweza kuwaelimisha na kutoa Ukombozi wa Ufahamu kwa dunia nzima.
“Ni kwa kutoa tu ndicho kinakufanya kile ulicho wewe”. (Ian Anderson)
Jitihada kwa ajili ya Amani
Rafiki yangu mkubwa aliuliza siku moja “Ina maana gani Kuwaanzisha na kuwapa Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho watu wengi kiasi hiki.” Sisi tulijibu kwamba Dunia iko katika hali mbaya na tunahitajika mno “kushusha” Nishati ya Kiroho kwa wakati huu. Kisha akauuliza
“Je, sisi tutaondoaje nia za wale ambao kila mara wanarudia na kusababisha vita katika dunia hii?”
Tulilazimika kuuliza Uongozi wa Kiroho moja kwa moja na hili ilikuwa jibu lao neno kwa neno.
Jibu lako lipo sio kwa jinsi gani kuondoa (nia ya vita) lakini jinsi ya kubadilisha fahamu ya Sayari yako. Mara baada ya tamaa ya madaraka inapogeuka kuwa uvamizi hakuna kitu cha kufanya. Kile tunacholenga sisi na kufanya ni kwenda kwenye chanzo na “psyche” ya binadamu kujaribu kuondoa hii jitihada iliyopo ya tamaa ya madaraka.
Siku zote kutakuwa na viongozi wa dunia ambao wanalazimika kufuata mahitaji ya wale ambao wanawatumikia. Tunachozungumzia ni watu wa kawaida ambao wanachafuliwa na kile mnachokiita “Dunia ya Kisasa”, ambayo kwa wakati huu ina maana uvamizi wa Teknolojia Mpya ambayo inavuruga akili na mawazo ya watoto wenu ambao ndio wazazi wa siku sijazo.Nini kinaweza kufanyika? Naam, kwa hali ya Kiroho tunaweza kuongeza fahamu lakini usiidharau nguvu ya taswira. Haichukui watu wengi kama unavyofikiria kuwa pamoja kama akili ya pamoja kuwazia maeneo yenye vita na kuondoa hofu, chuki na utafutaji wa madaraka kuwa upendo na msamaha.
Mawazo ya watu binafsi yana nguvu sana: ni nini kitatokea ikiwa akili zinazofanana zitajiunga kupambana kwa pamoja kwa ajili ya Wema? Mnaweza kuanzisha harakati kwa kutumia kundi lenu la watahajudi.
Nguvu Ya Taswira
Baada ya ujumbe huo hapo juu na kuhakikisha mambo fulani ya kiushirika tulifikia ifuatavyo:
Njia ya Kiroho ni ya maendeleo ya binafsi pamoja na huduma: hii ni fursa nzuri ya kuwatumikia binadamu. Tunaomba kwamba mara moja kwa wiki wakati wa muda wa kutahajudi kutumia baadhi ya muda kuwa na mtazamo wa kuelekea kwenye Kuwajali wengine, Upendo na Msamaha. Mara nyingi ni bora zaidi kufanya hivyo kwa pamoja katika kundi, lakini si mara zote inawezekana, hivyo bora kufanya hivyo mmoja mmoja kuliko kutofanya kabisa. Tunatumaini kuwa, kwa siku zijazo, idadi yetu inaongezeka siku zote kutakuwa na mtu fulani, mahali fulani mwenye maono ya amani kwa dunia wakati wowote
.
Ni muhimu kwamba matokeo ya tasira yetu wote iwe sawa; hivyo kusaidia, tumebuni mfululizo wa picha:
- Dikteta wazimu mwenye nguvu anachochea vurugu mbele ya watu wenye hasira.
- Maonyesho ya mawe, ukame, ardhi ya kijivu iliyoharibiwa na vita iliyoj na magofu, askari na milipuko ya risasi na silaha.
- Viungo vya miili vilivyokatwakatwa, watoto wanalia na akina mama wakiwa na huzuni.
- Mwanga mweupe ukitokea kwenye anga ya bluu na kubadilisha dunia katika mazingira mazuri na mimea ya kijani ambapo askari wanaweka silaha zao chini, wakilia na kukumbatiana.
- Wanawake na watoto huku wakicheka na kuwakimbilia askari waliotoka vitani.
- Watu wengi wanapiga muziki na kucheza / kuimba na kujenga vijiji na miji.
- Kiongozi mpya amesimama mbele ya umati mkubwa wa watu na kuahidi kwamba makosa ya zamani KAMWE hayatafanyika tena.
Watu ambao wanatahajudi kwa ujumla ni bora katika taswira, lakini hatupaswi kuwatenga wengine. Mtu yeyote anaweza kusaidia kwa jambo hili. Kwa hiyo tunawasihi muwaambie walio karibu nawe kuhusu taswira na kuwakaribisha kujiunga nasi. Kumbuka harakati zote huanza kidogo vinginevyo haziwawezi kukua! Tunasisitiza kwenu kwamba, kwa vyovyote vile, kile tunachoomba hakina motisha kuhusiana na kikundi cha kisiasa au imani za kidini.
Sisi tunasema hayo hapo juu kwa sababu CHANZO CHA HEKIMA ZAIDI kinatuongoza