Enlightenment Ndio Sababu ya Kuwepo Kwako

 
Umeongozwa kwenye tovuti hii….Hakuna kinachofanyika kwa bahati!
 

Ufahamu wa Kiroho ndio kusudi la mwisho la kuwepo kwako, lakini hadi hivi karibuni ulikuwa vigumu sana kupatikana. Ulikuwa unapatikana tu kwa “wateule wachache” na ulikuwa imefichwa katika mafundisho ya imani bila maswali (dogma), usiri na mtindo wa maisha….pesa kwa kawaida ilihusika vilevile!

Dhamira yetu ni kutoa Ufahamu wa Kiroho kwa watu wengi. Nguvu ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti na ugunduzi wa Hali za Ufahamu za Kiroho, zinapatikana kwa watu wote katika nchi zote, bila kujali jinsia, hadhi, tamaduni, jamii na imani.

Labda umekuwa na Uamsho, au labda unataka kutafuta njia ya kuanza kupata Nguvu za Kiroho mwenyewe.

Nguvu tunazozisema zinaweza kuchukua mfumo wa aina nyingi na kawaida huelezewa kama Nuru na Sauti ya Mungu. Hazifahamiki kupitia akili au kuumbwa na fikira. Zinapatikana katika Ngazi za juu za Ufahamu na zimeshuhudiwa na idadi kubwa ya watu miaka yote.

Tunapaswa pia kutaja kuwa watu wanaripoti kuwa na “hisia” ambazo zinaelezewa kama “Uwepo” mzuri wa Upendo na Amani.

Kila kitu tunachofanya ni bure kabisa bila wajibu wowote au mchango wa pesa. Tuko kama kikundi cha washirika ambao wanataka kufikia na kueneza Ukweli wa Kiroho kwa wale wote ambao wanahitaji msaada na mwongozo. Hatuombi chochote kama malipo na tunakataa michango yote. Hatuna kiongozi au majengo ya kutunza; Waalimu wetu wote hufanya kazi kwa uhuru.

Hakuna vizuizi vya mtindo wa maisha; tunawahimiza watu kujitunza wenyewe ili waweze kudumisha mazoezi mazuri ya Kutahajudi.
Tunapitisha Nguvu za Mwanga na Sauti kwa Wanaotafuta wa kweli na kuelezea kuwa sisi ni mifereji tu ya Nguvu hizi. Chanzo kiko katika Ngazi za Juu ambazo tunazitambua kama Viumbe ambao tunaowaita kama Uongozi wa Kiroho.

 

Uanzishwaji

Uanzishwaji ambao tunauzungumzia ni uhusiano wa kimiujiza ambao hufanywa kati ya Mtafuta na Ngazi za Kiroho. Hii inafanikishwa kwa “Kugusa” tu na mmoja wa Walimu wetu. Mwalimu ni mtu ambaye amefuata Njia ya Mwanga na Sauti na kupata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Muunganisho huu ni wa kudumu lakini unahitaji mazoezi ya mara kwa mara ya Kutahajudi ili kuongeza na kukuza faida yake.

Nguvu hizi za Mungu zipo kukuongoza kwenye Njia ya Kiroho na Kukufundisha mafunzo unayohitaji kujifunza. Ufunuo wa kuvutia wa Ajabu, zaidi ya mawazo yote, hufunuliwa na mwishowe zinaweza kukupeleka kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.

 

Uamsho

Nishati ya Kiroho kwenye Sayari hii iko katika kiwango cha juu sana kwa wakati huu. Hii inamaanisha kwamba idadi kubwa ya watu kote ulimwenguni wanapata Uamsho wa kushangaza bila kutegemea, wengine wanapata hata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Mara nyingi Uzoefu huu ni wa ajabu sana hivi kwamba watu wanakuwa na mashaka kuwa ni halisi. Tunafurahi wakati wowote kutoa ushauri, ambao kwa mara nyingine tena, ni bure kabisa, na kutoa wasiwasi wowote. Tunaona Uamsho huu kama kidokezo cha kitu kikubwa… Njia ya Kiroho inayofikia mwisho katika Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.

Tunayo tovuti nyingine ambayo inazingatia Uamsho na Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Ina Ushuhuda wa kushangaza, mwingi kutoka kwa watu ambao hawajawahi hata kutahajudi.


www.awakeningenlightenment.com

 


 

Ukombozi Wa Ufahamu au Enlightenment

Neno hili limetumika katika enzi zote na hubeba wigo mzima wa maana. Kwa hivyo ni muhimu kufahamisha haswa kile tunachomaanisha na Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment. Kwa hivyo tumechukua ukurasa mzima wa tovuti hii kuifafanua, na kuweka ushuhuda wa watu ambao tumewasaidia kupata Hali hii.

Kwa sasa tutasema tu kwamba Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au Enlightenment ya kweli ya Kiroho hufanyika wakati mtu anapoungana na Umoja na kupoteza kabisa ubinafsi wake au kile anachojua na yeye.

 

Uongozi Wa Kiroho

Mnamo Februari mwaka 2015 idadi ndogo ya Watahajudi ambao walikuwa wapepata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment walipata mawasiliano na Uongozi wa Kiroho. Viumbe hawa wametokea mara nyingi huko nyuma. Wakati mwingine kwa watu binafsi na wakati mwingine kwa vikundi kama vile Theosophical Society ambao waliunda jina, Uongozi wa Kiroho au Spiritual Hierarchy.

Kusudi kawaida ni kusaidia kumwongoza mtu binafsi, au kutoa maarifa kusaidia binadamu. Nguvu za Kiroho zinafunuliwa kwa watu wa Sayari hii kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tena! Tunauita muujiza huu kwa jina la Lightwave Mpya.

Tunayo tovuti nyingine ambayo imewekwa maalum kwa ajili ya Uongozi Wa Kiroho. Ina Ujumbe mwingi toka kwao ambao unavutia kusoma.


www.spiritualhierarchy.com

 

Dunia Nzima

Ukurasa wa Dunia Nzima una mwaliko wa wazi kwa Watahajudi, kote Duniani, kuungana nasi katika kutuma Upendo na Mwanga kwenye Sayari yetu ya thamani. Ni muhimu sana kuamka na kushughulikia maswala ambayo yanatishia idadi kubwa ya viumbe na mimea ambyo inaishi kwenye Dunia yetu hii nzuri. Tunahitaji sana kurejesha usawa na uelewano haraka iwezekanavyo.
 

Msukumo

Watu ambao wanatafuta Ukweli mara nyingi wanahitaji uhakikisho kuwa kuna wengine ambao wana Jitihada sawa. Watu wengi wanatembea kwenye Njia ya Kiroho, lakini inaweza kuwa na upweke kwani lazima Utembee peke yako. Ni muhimu kuzingatia na nidhamu kudumishwa ikiwa mtu anataka kufikia Lengo lake.

Kwa hivyo tunatoa makala kadhaa za kusaidia kukuza na kumhamasisha mtu kwenye Njia ya Kiroho. Ufahamu wa Kiroho haipatikani kamwe kwa maneno lakini maneno ni muhimu sana kumwelekeza mtu kuelekea kwenye mwelekeo sahihi.

 

Ushuhuda

Ikiwa unaanza safari unataka kujua kuwa njia uliyochagua itakuongoza na kukufikisha mwisho wa Safari yako. Cha kushangaza, ikiwa unafuta Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment huwezi kujua Mwisho wa Safari kabla hujafika. Unaweza kusoma maelezo lakini unahitaji kuamini kuwa hiki ndicho haswa Unachotafuta!

Kwa hivyo tumekusanya Ushuhuda mbali mbali kutoka kwa watu ambao waliopata Uamsho bila kutegemea na / au wametahajudi kwenye Nguvu za Mwanga na Sauti. Tumejumuisha pia Ujumbe mchache kutoka kwa watu waliopata Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment na Walioacha maisha yao ya Duniani na Kupanda kwenda kwenye Ngazi za Kiroho.

 

Ukurasa Wa Mawasiliano

Tumetoa ukurasa wa mawasiliano ili uweze kuwauliza Walimu wetu maswali yoyote yanayohusiana na Elimu ya Kiroho na Kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ya Mungu.
Wasiliana na Walimu wa Kutahajudi
 
Tunapenda kumshukuru Amanda Sage kwa huruma na ruhusa yake ya kutumia picha nzuri ya Limbic Resonance inayoonyesha Uhamisho wa Nishati ya Kiroho kati ya wanadamu. www.amandasage.com