Punzi/Mantra

Kutahajudi Kwa Pumzi

 
Hii hutumika kuendeleza lengo (focus) na dhamira na inapendekezwa kwenye hatua zote za safari.

Faida Zake:

• Husaidia kupumzika na kuleta amani na utulivu
• Inasaidia usitawanyike ila uwe katikati
• Kukuza afya na hali ya ustawi

Kutahajudi kwa kupumua, kukifanywa vizuri, kunaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa na kusadia aina za juu za kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti.

Kutahajudi pengine ndio jambo la changamoto kubwa ambalo utawahi kufanya katika maisha yako yote, na kitu chochote ambacho hufanya kazi hii kuwa rahisi lazima kikubaliwe. Mtu anahitaji kupumua vizuri kujiandaa kwa ajili ya, na wakati wa, mawasiliano na nguvu za Mwanga na Sauti ya Kiroho.

Kwa yule anayeanza mwanzo kabisa tunashauri kuangalia / kusikiliza video za YouTube. Hii itakuongoza wewe hatua kwa hatua katika mbinu hii ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu mkao, akili na kutumia mwelekeo (focus). Hii ni njia rahisi ambayo inazawadisha na ya kuanza kutahajudi, na mamilioni ya watu duniani wanafanya zoezi hili.

 

 

Kwa kuanzia tunaweza kupendekeza sauti (audio) ya Lori Granger inayoitwa ‘Sitting with Breath’ ambayo inamfaa mtu anayeanza na itakuongoza kwa kikao cha muda wa dakika 15. Wakati unasikiliza sauti hii unaweza kutumia na kuangalia moto wa mshumaa kama mahali pa lengo lako (focus): watu wengi huona zoezi hili kuwa zuri na la kutuliza pamoja na kufurahisha sana. Kadiri ya uwezo wako na kujiamini kunavyoongezeka utakuwa na uwezo wa kutahajudi kwa pumzi bila matumizi ya mshumaa: itakuwa ni sehemu ya asili ya ratiba yako ya kila siku. Kupata sauti (audio) ya kutahajudi bonyeza tu kifungo hapa chini:

Sitting with the Breath: A Meditation by Lori Granger

Hatimaye tutatengeneza video yetu na tutakujulisha wakati itakapopatikana. Endelea kuangalia hii tovuti.
 

Ushuhuda (A.H.)

 
Mimi ni (A) naandika ili kuwaeleza uzoefu wangu. Kwanza ningependa kusema kuwa uzoefu wangu wa kutahajudi ulikuwa mzuri. Ulinichukua kwenye maeneo tofauti ambapo nilikutana na mabwana na jamii za mwanga ambao wote ulikuwa mweupe. Nilijisikia kama undugu wa aina fulani, ubatizo wa moto, wa mwanga wa ndani nk. Pia nilihisi kama mwili wangu ulijazwa mwanga, seli zangu zote zilikuwa zinakandwa na kwamba nilikuwa na uwezo wa kufanya na kuonyesha kitu chochote katika ulinganifu na mwanga. Nilijihisi niko nyumbani na nguvu kama kila kitu kilikuwa ninakijua wakati nikiwa kwnye kutahajudi.
 
Kumb. Ushuhuda huu ulikuwa unatoka kwa mtahajudi ambaye alipokea moja ya Mantra yetu; bado hajaanzishwa kwenye Nguvu za Mwanga na Sauti.

 
 

Kutahajudi Kwa Mantra

 
Utakapojisikia unaweza kutahajudi na pumzi vizuri hatua inayofuata ni kuomba mantra ya binafsi – unaweza kuwasiliana nasi hapa.

Mantra ni seti ya silabi iliyoundwa kufanya usawa kwenye mwili, hisia na akili ili kumwandaa ‟mtafutaji” wa aina ya juu ya kutahajudi.

Mantra ya binafsi kwa kawaida ni silabi 3 na hizi husemwa kimya kimya kwa ndani na kwa nguvu kwa nia ya kulenga (focus). Mantra HAZITAKIWI kuoaniswa na pumzi. Huenda utaanza kwa njia hiyo lakini acha pumzi iendelee kwa wakati wake na wewe endelea ‘kutaja kimya kimya’ silabi za mantra bila kuchoka.

Kwa awali, kwa wale ambao hawajawahi kufanya taamuli ya Mantra, wajaribu dakika 5-10. Mkao wowote ambapo mgongo umenyooka kwenda juu ni kamilifu kabisa. Hata hivyo, kwa wale ambao wanataka kukaa mkao MaYogi tafadhali mjisikie huru kufanya hivyo! La muhimu ni kwamba unaweka ufahamu wako kwenye mantra na sio kwenye usumbufu wa maumbile. Unahitaji kuwa katika nafasi ya utulivu, bila ya usumbufu: ni muhimu kuwa na sehemu maalum na muda wa kila siku kufanya tahajudi hii.

mantra meditation

Wakati wa kutumia mantra sheria za tahajudi ya pumzi bado zinatumika pia. Utaona kwamba akili yako inatawanyika na kujigundua kuwa unafikiri “mawazo ya siku nzima”. Hii ni kawaida kabisa: sasa una uchaguzi, na unapaswa kuwa mpole na kurudi kuendelea na mantra. Jaribu kutojali sana kuwa umetawanyika kwani kufanya hivyo kutavuruga utulivu wa tahajudi yako.

Kabla ya kuomba kufikiriwa kwa ajili ya kuazishwa mtu anapaswa kutahajudi kwenye Pumzi na Mantra. Hasa anatakiwa kujenga tahajudi zake na kufikia saa moja kila siku. Kama unapenda kuanzishwa wasiliana nasi hapa.

Hakuna malipo kabisa ya mantra au kuanzishwa ‘initiations’ (tazama ukurasa juu ya kutoa).