Ushuhuda (L.A.)

 

Kuzungumza juu ya jinsi UZOEFU huu mzuri ulivyotokea, ni kurudi kwenye Kuanzishwa kwenye MWANGA NA SAUTI, ambapo nilifika kwa kufuatia moyo wangu. Ilikuwa ni uhusiano na uzima, nilihisi sehemu na wakati huo huo kila kitu, ilikuwa ni hisia isiyoelezeka, ngumu zaidi kwa sababu mimi nilikuwa mtu wa mwisho kusimulia uzoefu wangu, kwani kwa mawasiliano walianza upande wa pili wa duara ambalo tulikuwa tumetengeneza. Nilisikiliza uzoefu mzuri wa mwanga wa rangi, za kuonekana kwa Mabwana katika Tahajudi.

Hoja yangu ilikuwa juu ya Ulimwengu mkubwa na wa ajabu bila rangi na zaidi ya kuona, ilikuwa ni kuhisi, kila kitu kilikuwa kizuri.

Baada ya karibu mwaka mmoja, kabla sijaweza kuonana, na kabla hata siwezi kuongea na (C), ambaye alikuwa Mwalimu ambaye alinianzisha, nilihisi kuwa naogopa … niliogopa kutostahili kupata Enlightenment, nilikuwa nikisikia moyoni mwangu wito ambao ulituliza mawazo yangu, baada ya hapo niliamua kumpigia simu.

Hapo ndipo aliponiuliza ni lini tunaweza kukutana ili kufanya mchakato maalum wa kumaliza mchakato wangu wa Kiroho na ndipo tukakubaliana mahali, siku na wakati wa kukutana.

Ilikuwa mchana wenye joto zuri, nilitembea kutoka nyumbani kwenda mahali pa mkutano, nikitembea kwa umakini na kwa moyo wazi kwa chochote ambacho mkutano huu na yeye utakuwa. Ulifanyika nyumbani kwa (L), kiumbe mzuri aliyepata Enlightenment mwenye Nafsi ya Muujiza na mwenyeji wa nyumba iliyojaa Nuru. Tulianza kwa undani uchunguzi mzito na tukiongozwa na Mwalimu na mara moja unganisho hili lilipita na kupanuliwa kwa njia ya ajabu, ilikuwa sawa na uzoefu ambao tayari niliupata kwenye Kuanzishwa, ingawa uliongezeka kwa nguvu hadi mara kumi na mbili, ilikuwa uthibitisho wa ajabu, ufunuo, Ilikuwa ajabu, Kuwa kwangu kukawa Upendo wa Kiulimwengu (Universal Love). Mwishowe, niliunganika na kukumbatiana na (C) na (L), pamoja na mimea mizuri ya nyumba hiyo ambayo ilicheza kwa furaha kwa wakati ule wa Muujiza. Nilijiona nikipungua, nikimtazama (C) na kuona macho yake yamejaa Mwanga Mweupe na ndipo nikagundua kuwa tulikuwa Mmoja, wote ni Mmoja, Umoja wa Ajabu, Sasa kwa kuwa ninajaribu kuielezea najua hakuna maneno, nilikuwa na furaha.

Baada ya siku nane za uzoefu huu, nilikutana nae tena kufanya matibabu na bakuli za ki“Tibeti”, tukazungumza, nikamwelezea kuhusu kutahajudi kwangu, jinsi nilivyofurahia nafasi hiyo kuungana na ule Umoja, tukaanza matibabu na kisha uzoefu wangu wa tatu ukaanza kwa ajabu, ukazidi kwa mara nyingi zaidi ule uzoefu wa siku 8 zilizopita.

Katika uzoefu huu nilibebwa ndani ya mfumo wangu wote wa seli, atomi na molekuli, nikahisi vitu vizuri vya ajabu, kupokea habari na uthibitisho, nilipanuliwa bila kuwa na mwisho (to Infinity), niliunganisha na “Ubinafsi” Kamili. Nilikuwa ndiyo Kile. Ilikuwa ni uzoefu usio elezeka, uzoefu uliojaa rangi, za chakras, za seli, za ufunuo wa sasa, ulipanuka ndani ya indigo ambayo ilinipunguza, ikapanuka na kupanuka tena na nikawa Upendo.

Sasa najua kuwa nimepata uzoefu mzuri sana wa maisha yangu yote.

Kwa ushuhuda huu, nataka kusaidia kukuhimiza kuungana na Mwanga na Sauti, kwa hakika ya kwamba ni Njia nzuri ya unganisho kamili na Chanzo cha Uumbaji wote na uwepo wa mwanadamu.

Nawapenda! ❤