Ukweli Kuhusu ‟Enlightenment”

 

Mara nyingi ikijulikana kama hali ya kudumu ya kuwa.

Kutoka Uongozi wa Kiroho

Hali ya kudumu ambayo mnaisema haiwezi kuwa ya kudumu, katika mwili wa kimwili. Unaweza kuwa na ‟realizations” pamoja na hali za ufahamu lakini hivyo ndivyo zilivyo, sio hali za kuwa.

Kwa mfano, unaweza kushuhudia hali ya “kutokufikiri” kwenye kina cha tahajudi, lakini wewe ni shahidi, sio ile hali.

Kwenye ‟Enlightenment” unakwenda kwenye ile “hali ya kudumu” kwa muda, na kujisikia tofauti na maisha yatabadilika kwako – lakini unarudi kuishi maisha yako, angalau kwa mtazamo tofauti. Narudia tena, UNARUDI, inakubidi, ama sivyo huwezi kufanya kazi na kuwa kama binadamu.

Mtu mwenye ‟Enlightenment” akifa kwanza anavua na kuachia gamba la kimwili, na kupanda kwenye ngazi za juu na kuingia kwenye “usingizi mzito” wakati anaendelea kuvua miili zaidi ambayo ilitumika wakati akiwa katika mwili wa kibinadamu duniani. Kisha mabadiliko hutokea na “yeye” sio tena “mtu binafsi” lakini bado ana ufahamu, Kiumbe wa Mwanga. Kiumbe wa Mwanga sasa anajiunga na Kiini ‟Essence” chake ambacho daima kinaishi kwenye Ulimwengu wa Kiroho ..

Kufuatia hii kuna vitu 3 vinavyowezekana:

1) Kuunganika kwenye Umoja …… .daima.

2) Kukaa katika Ulimwengu za Kiroho, kuhudumia na kuendelea kujifunza.

3) Kurudi kwenye ngazi za kimwili kwa kuchukua seti nyingine ya miili na kuendelea kujifunza zaidi masomo ya maisha.

Ujumbe huo hapo juu unatoka moja kwa moja kutoka Uongozi wa Kiroho lakini tunahisi baadhi ya mambo yaliyopo yana haja ya kuelezea zaidi:

Baadhi ya walimu wa Kiroho hudai kwamba ‟Enlightenment” ni hali ya kudumu inayopatikana kwa mtahajudi na mara inapopatikana haiwezekani kamwe kujitenga. Tumeambiwa kuwa hii sio kweli: tunaweza kuwa na uzoefu na hali hii kisha lazima kurejea kwenye akili na hisia. Mtahajudi nzuri anaweza bila shaka kurudi kwenye hali hiyo mara kwa mara.

Kielelezo kinachopatikana katika falsafa nyingi za dini ni Roho ‟Soul”: – sehemu ya kudumu ya ubinafsi ambayo haifi wakati wa kifo cha kimwili. Hii inajulikana na Uongozi kama Kiumbe wa Mwanga. Na huungana na Kiini chake ‟Essence”, hivyo inaonyesha kwamba Roho ‟Soul”: ni sehemu ya Ubinafsi ya kweli. Kiini Hiki ‟Essence” kinabakia kwenye ngazi za Kiroho, wakati Roho ‟Soul”: inachukua mfululizo wa magamba mbalimbali kuiwezesha kuweza kuwa na kuwepo kimwili.

Je kuhusu watu ambao bado hawakupata ‟Enlightenment” wakati wa maisha yao? Wakati wa kifo cha mwili, wao pia watakuwa Viumbe wa Mwanga, na kubaki katika ulimwengu wa Kiroho kwa muda, mpaka Roho ‟Soul”: ilazimike kuchukua mwili mwingine wa kimwili. Mchakato mzima inaonekana hutegemea kujifunza, sio elimu ya kawaida ya shuleni tu lakini masomo ya maisha, hasa yale yanayohusiana na mahusiano na watu wengine. Jinsi ambayo mtu amesafiri zaidi kwenye Njia ya Kiroho, ndio uwezekano wa kubaki zaidi katika ulimwengu wa Mbinguni unavyozidi, ambapo tena kujifunza kunafanyika.

”Enlightenment” ni mada mkubwa na ya kushangaza, na tunatambua kwamba huu ni muhtasari mfupi tu wa somo lenyewe. Tafadhali tutumie maswali na tutajitahidi kuyajibu kwenye sehemu ya Maswali na Majibu.