Uongozi Wa Kiroho

Ili kuelewa ni nini au ni nani Uongozi Wa Kiroho, tunahitaji kwanza kuangalia siku za nyuma. Historia inaonyesha kwamba Elimu Ya Kiroho ilikuja duniani kwa njia ya walimu wakuu, walimu wenye miujiza, na waliobobea na mara nyingi ikaishia kuwa dini. Kwa bahati mbaya Ukweli ulipotea kwa sababu ya ”Ego”, ulafi na tamaa ya madaraka nk. Safari hii tunaambiwa kuwa ni lazima UKWELI WA KIROHO uwafikie watu wote. Hivyo ni lazima kujifunza kutoka kwenye historia na kuhakikisha kwamba Ukweli wa Kiroho unapatikana iwezekanavyo na mafundisho yawe wazi kabisa.

Hii haitakuwa Njia kwa watu wachache waliochaguliwa lakini ni Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho “Enlightenment” kwa ajili ya watu wote. Wengi wenu mnawezi kufikiria kuwa hamna hali ya Kiroho lakini kama umewahi kuhoji kuhusu kuwepo kwako au kuhisi ndani ya moyo wako kuwa kuna sehemu yako wewe inakosekana, basi Njia hii ni kwa ajili yako. Kinachotakiwa kwako ni kujifunza mazoezi ya kutahajudi, kuwa na maisha ya afya na muhimu zaidi kujifunza jinsi ya kutoa kwa dhati.

Kwa wale ambao wanataka kupokea lazima kwanza wawe na uwezo wa kutoa. Tunaamini kwamba Uongozi wa Kiroho wako nyuma ya ”Masters” wote na Dini zote ambazo zimewahi kujulikana. Wanahusika kwa ujenzi wa Mapiramidi, kuzuka kwa ustaarabu na mafanikio mkubwa katika sayansi ya kisasa. Wengi watashuhudia kuwepo kwao kama manabii, waonaji, “mystics”, “clairvoyants” na watu walio na mwanga wa uongozi au ubunifu na kama wakiwa waaminifu na bila “ego” wanashuhudia kuwa haikuwa wao: “Ilinilazimu tu” au “mawazo yalikuja tu kichwani kwangu”.

Kwa wakati huu watu wachache ambao wamepata hali za Kiroho za juu wamewasiliana na Uongozi wa Kiroho kwani wana ujuzi muhimu na Ufahamu wa juu, na kuweza kutoa Ufahamu wa juu kwa wengine. Watu hawa wanataka kufanya kazi kama Uongozi wa Kiroho wanavyofanya, kuwa nyuma bila tamaa kuwa kwenye shirika kubwa. Wao wanaahidi kujishughulisha maisha yao yote kwa ajili hii. Wao wameshangazwa na mambo ambayo wamesikia na wamekubali kwa unyenyekevu kwamba wamechaguliwa, ili kutoa Elimu hii na Ufahamu wa Kiroho. Kwao hakuna kitu kingine cha muhimu na kikubwa zaidi.

Limetolewa ombi kuwa tukusanye mahali pamoja maandiko yote yaliyo toka kwa Uongozi wa Kiroho na kuyaonyesha. Maandiko mengi yametolewa katika makala, ambazo nyingi zinapatikana kwenye ukurasa wa Msukumo.

Kutokea hapa tulipokaa sisi, kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, imekuwa muhimu kuleta chini kiasi kikubwa cha Nguvu ya kushughulikia kukosekana kwa usawa wa dunia. Kuna wengi wenu tayari wanasaidia katika kazi hii. Tunachoomba ni kuwa watu waangalie mioyoni mwao na kuleta mabadiliko makubwa kwa kushughulikia masuala matatu makubwa:

KUKUBALIKA, UPENDO, MSAMAHA

Kwa masuala hayo matatu yakiwa muhimu kwenye akili za watu dunia yenu itasaidiwa mno kuzidi kipimo chochote kile.
 
 

“Je, umeshawahi kujiuliza in jinsi gani Kweli mwili unaweza kutembea; mnyama wa uzito wa tani, jinsi gani huu uzito mkubwa hujichukua wenyewe kutembea? Maajabu ya Dunia ni makubwa sana kuyatafakari lakini ningependa ujaribu – jaribu kutambua jinsi ambavyo Wanadamu wamelemaa na kukubali tu mambo kama walivyoyakuta bila kustaajabu, kuwa ni kwa namna Gani na Kwa nini.

Ni muhimu kufanya hivyo na kisha kuendelea na swali kubwa zaidi linalofuata, “Kwa nini Mungu kwa ufanisi Aweke watu duniani na kutojua kwao alafu anawatarajia kutambua Asili yao ya kweli na hatimaye kurudi kwa Mungu?”

Watu wengi hawajui hili na hupitia maisha wakiwa kwenye giza la Kiroho kabisa hadi mwisho wa siku zao kama walivyoanza, katika Ujinga wa Asili yao ya Kiroho. Jibu la swali hili, kama kawaida, ni kuwaambia watu kwamba njia pekee ya kweli kujua (jibu) ni Kutahajudi na kupata Njia ya Kweli ya Ndani ya Mwanga na Sauti.

Tangu mwanzo wa wakati imekuwa njia hii. Nazungumzia kabla ya maarifa yoyote na ustaarabu wote uliopita.

Ulimwengu, pamoja na Mikusanyiko ya Nyota ”Galaxies” zote na Nyota zina siri nyingi ambazo hatua kwa hatua zinajitokeza na kugunduliwa. Lakini bado kuna hatua ndefu ya kwenda tunapokuwa kwenye mwili. Hata hivyo, kama mtu akiwezeshwa kuwa na Ufahamu wa Kiroho kwa kupitia Kutahajudi anaweza ”kwenda” kwenye Uumbaji na kugundua mwenyewe siri na maajabu haya.”

Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kutoka Uongozi wa Kiroho

Click here for more transmissions from the Spiritual Hierarchy