Neema

 

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeona maelfu ya watu kote Duniani Wakianzishwa kwenye Mwanga na Sauti.

Kijadi, Safari ya Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment ilikuwa ngumu sana na ilimtaka Mtafutaji kufuata mtindo wa maisha magumu ya kujizuia; wengi wangeshindwa kufikia Lengo lao. Siku hizi Njia imetolewa kwa umati na idadi kubwa ya Walioanzishwa au Initiates wamepata safari hiyo moja kwa moja, ili mradi wanaanza na kudumisha mazoezi ya Kutahajudi mara kwa mara.

Hata hivyo, wachache wamekuwa na ugumu wa kuwa na maendeleo na wamejiuliza ni kwanini! Kuna majibu dhahiri kwa swali hili na mengine ambayo sio!

Kama ilivyoelezwa hapo juu, mtu anahitaji kujifunza jinsi ya Kutahajudi; hiyo sio sawa na kukaa tu juu ya mto. Inahitaji kujitolea, mazoezi, uvumilivu na uwezo wa kujiachia tu. Watu ambao wana tamaa sana ya Hali za Kiroho au wanataka kubaki katika kudhibiti kila kitu pia watakuwa na ugumu kuendelea.

Sababu ambazo hazionekani wazi zinaweza kuhusisha maisha ya zamani: Ikiwa mtu alikuwa ameanzishwa hapo awali wataona ni rahisi sana Kutahajudi katika maisha haya. Watu ambao wamekuwa katika vikundi vingine wanaweza kupata shida kukubali Mafundisho ya Uongozi wa Kiroho na kujipanga, kukubaliana na Wimbi Mwanga (Lightwave) Mpya. Inaweza pia kutegemea na Karma, ambayo tunaambiwa haiwezekani kwetu kuelewa kikamilifu. Hata hivyo, kuna jambo lingine, labda la muhimu zaidi, ambalo ni rahisi kupuuzwa.

Hapa ni Mabwana wa Mwanga.
Swali ulilouliza linaanza na kuishia kwa NEEMA: “kutabasaniwa” na Uwepo au Nguvu kubwa kuliko wewe.
Hakuna kustahili Hali za Kiroho, angalau kwa njia ambayo neno linaeleweka kwa wanadamu.
Na sio kuhusu Tamaa pia, kwa kweli tamaa inaweza kuwa kizuizi.
Kwa hivyo tumebaki na:
Hakuna Tamaa
Hakuna Kitendo
Hakuna Kujitahidi
Kuwa tu – tayari kwa chochote kinachokuja!

Kumbuka kuwa ikiwa unaona umekwama, huko peke yako. Uliza msaada kutoka kwa Uongozi wa Kiroho na pia washauri wako, ambao wako tayari kukupa msaada na ushauri kila wakati.