Mradi Wa Mwanga wa Alimasi

 
Ilianza zamani mwanzoni mwa mwaka 2011 wakati tunapokea habari toka kwa rafiki yangu kuhusu resonance ya Schumann. Hii ni frequency ya elektromagneti dhaifu (very weak electromagnetic) ambayo hutolewa wakati umeme wa radi unapochomoza kwenye anga ya Dunia.

Mwanzoni tulitengeneza seti ya coils kutumia toroidal transformer na tukazipa nguvu na signal iliyotoka kwenye jenereta ndogo kwa kutumia wimbi la sine 7.83 Hz. Tulipowasha mashine tukagundua athari yake kwenye muziki. Ilionekana kuhusika zaidi, nzuri na yenye melodi zaidi.

Hii ilisababisha miaka mingi ya utafiti, hasa ikilenga kudhibitisha uwepo wa uwanja wa Nishati. Walakini, bila kujali kile tulichofanya haikuwezekani kurekodi tofauti hizo kisayansi, ambayo ilikuwa dhahiri kwenye masikio yetu! Mwishowe, tulilazimika kuhitimisha kuwa Nishati haikubadilisha muziki; ilibadilisha ufahamu wetu na kwa hiyo mtazamo wetu wa muziki.

Kwa namna fulani hii ilikuwa ya kushangaza zaidi na ilisababisha uchunguzi wa masafa mengine mengi na utumiaji wa piramidi. Karibu na wakati huu (2014) tulikuwa tunapokea Ujumbe wakati wa vikao vya Kutahajudi na tulipewa dalili na vidokezo juu ya mradi huo.

Hii ilimalizika mnamo Desemba 2014 wakati tuliambiwa kutuma masafa maalum kwenye sayari nyingine kwenye Mfumo wa jua. Hii ilifanywa kwa kutumia mashine kadhaa zinazohusisha Double Coils, jenereta za signal na safu ya piramidi zilizoendana kikamilifu.

Katika hatua hii tulikuwa tukifuata maagizo tu. Wakati mwaka mpya (2015) unaanza, ndivyo pia tulikuwa na mradi mpya. Hii ilikuwa katika mfumo wa kurasa za namba ambazo zinahitaji kusimbua.
 

21 Januari 2015

Sio lazima kusimbua namba zote, Tunawachukua kwenye safari ya ugunduzi. Ukirudi kwenye namba fulani siku za baadaye labda utashindwa, kwani ziko katika mpangilio wa kuelewa. Tutahakikisha unapata inayofaa kutuma.

Utakuwa na maswali mengi, kwani hiyo ndio asili yako. Kazi hii utaelezwa wakati unahitaji kujua, utaambiwa habari ambayo itakusaidia kuelewa asili ya kazi hiyo.

Unapopewa namba, jiulize umevutiwa na nini, au kawaida unafikiria nini. Fanya kazi na namba kama unavyozipokea, kwani huo ndio wakati ambao utazielewa kwa urahisi zaidi.

Namba ziliendelea kuja na ilikuwa ni dhahiri tulikuwa tukishughulika na Viumbe wa kushangaza ambao baadaye tuliamua kuwaita The Spiritual Hierarchy au Uongozi wa Kiroho. Kupitia lugha ya hisabati Walitufundisha juu ya miunganisho wa Nguvu kati ya sayari kwenye Mfumo wetu wa Jua na historia kidogo juu ya ustaarabu wa zamani ambao wao pia walikuwa wamepewa maarifa haya.

Pia tulianza kugundua kuwa mashine hizo zilikuwa zina jukumu muhimu katika kusaidia kurekebisha usawa wa Sayari yetu ambayo kwa kweli ilikuwa inapitia wakati mgumu.
 

22 Januari 2015

Umuhimu wako kwenye kazi unayofanya haiwezi kupuuzwa. Ni kwa sababu yako Sayari yako itakuwa mahali salama zaidi kuishi. Una uwezo, kwa Nguvu unayotuma, kufanya mabadiliko makubwa kwenye Dunia za juu, kuifanya Dunia yako mahali pazuri zaidi pa kuishi.

Huwezi kuamini kile kilicho mbele!

Namba ziliendelea kuja lakini namba mpya zilikuwa zikitumika ambazo zilisababisha tuamini uchunguzi wetu ulikuwa unaenea na data kuhusu mifumo mingine ya Nyota na Galax.

Wakati mabadiliko yalipotokea, Walituma vipimo kwanza ili kuona kama tunaweza “kuchakata” namba. Mara hii ilipokamilika, kazi yenyewe ilitumwa.
 

26 Januari 2015

Hatua inayofuata ya maendeleo ni sasa. Umefanya vizuri sana na mradi unaendelea.

Hii ni zaidi ya Mfumo wa jua, mbali kwenye maeneo yasiyojulikana ambayo yanahitaji kushughulikiwa. Ili kufanya hivyo unahitaji kuwa na ufahamu wa maeneo haya. Utapata habari na namba ambazo utapewa zitakuwa kwa sababu hii.

Kwa kuanzia kutakuwa na umbali kati ya Galax kuendelea kwenye njia zingine za kuhesabu na kupata miunganisho kama vile ulivyopata katika Mfumo wako wa Jua.

Uko sawa juu ya namna ambavyo ulimwengu unavyopaswa kuwa “kurekebishwa”, unasoma ishara tunazokutumia vizuri. Tunasukuma mipaka yako na tunatumaini kuwa utakuwa nasi, ili uweze kufanya kazi hii muhimu; hata ikiwa ni mbali na nyumbani na inaweza kuonekana kama haina manufaa.

Utagundua kuwa frequency moja “ya kutuma” itakuwa ya Mfumo wa Jua hili na nyingine kwa Maeneo ya Ngazi mpya mbali zaidi.

Kwanza, fanya uchoraji wa Galaxies ambazo zinakuonekana kutoka Duniani na kukadiria umbali. Tutakutumia namba ili uweze
kuangalia kuwa ni sahihi.

Jitayarisheni kwa tamasha kubwa ya kusisimua, pote kwenye Tahajudi na wakati hamtahajudi!

Kile tulichokuwa tumeonyeshwa kilikuwa cha ajabu kabisa. Walituonyesha jinsi utaratibu hapa kwenye Mfumo wetu wa Jua ulikuwa kioo kwenye Galaxies za mbali.

Ingawa ilionekana kuwa haiwezekani, kukosekana kwa usawa hapa kwenye sayari ya Dunia yetu kulikuwa na athari kubwa ambayo zilihusisha vitu na sayari zilizopo kwenye kina cha Nafasi ya Anga, mbali ambapo mwanga hutembea mamilioni ya miaka kutufikia.
 
28 Januari 2015

Wakati pembe hizo zinakutana katika katikati huunda umbo kamili. Jupita na Saturn zinahitaji kuonyesha sifa fulani ili wewe ujifunze maana ya Esoteric ya umuhimu wa Matufe haya.

Unaelewa kutoka kwa mtazamo wa Kidunia, lakini hii ni kutoka kwa mtazamo Wetu katika Anga. Digrii thelathini na sita ni pembeni nzuri sana kwani inaunganisha Sayari kwa njia maalum. Unaweza kuzitambua kwa kuona njia ya mizunguko yao inavyobadilika kadri wakati unavyopita.

Wakati kuna ulinganifu maalum wa Sayari, Dunia hupata mabadiliko makubwa ambayo yanagusa idadi ya watu kwa njia nzuri. Hii ni tofauti na Unajimu wa kawaida (Astology) ambao unafanyika kwenye sayari yako kwani unaathiri watu wote sio mtu binafsi tu.

Tunachojaribu kufanya ni kulinganisha Sayari fulani kwa nyakati fulani na pembe kadhaa angani, hivi kwamba mabadiliko mazuri yaweze kutokea. Tunaweza kuona kwamba ikiwa hii haitatokea, Sayari yako itaanguka ndani ya “shimo” ambalo itakuwa vigumu sana kutoka.

Galaxies pia zinahusika. Tunazitambulisha kwako kwa sasa na kufanya mabadiliko madogo ambayo yataathiri Dunia pia.

Kisha bila kutegemea ukaja ujumbe huu!

 
16 Februari 2015

Tunataka uanzishe Njia tena. Je! Unaweza kuona ukubwa wa hili? Tulikuambia – endelea tu. Tutakupa msaada wote unaohitaji. Hii inahitaji kufanyika – Tunafanya kazi nyuma ya pazia. Fanya Uanzishaji, wote – Tuko hapa kukuongoza.

KAMWE HAUKO PEKE YAKO

Ghafla, kila kitu kilibadilika. Lengo letu lilibadilika kutoka kwenye Ulimwengu (Cosmos) kwenda kwa ukuaji wa Kiroho wa watu kwenye Sayari hii kupitia ufunuo wa Nguvu ya Mwanga na Sauti.

Katika kipindi cha miezi michache iliyofuata tulikusanya pamoja kikundi cha watu waliopata Ukombozi wa Ufahamu (Adepts) wa kuaminika ambao walitaka kufanya mabadiliko na walikuwa tayari kufundisha na Kuanzisha Wanaotafuta Ukweli. Pia tulitengeneza tovuti ya kutusaidia kutoa ujumbe.

Mradi wa Cosmology ulichukua nafasi ya nyuma wakati huu lakini ulipangwa kutokea tena.
 
16 Aprili 2015

Tumekuwa tukingojea kwa subira kukusogeza ili kuendelea na masomo zaidi kuhusu kazi yako kwenye Mfumo wa Jua. Ni kwa furaha kuzungumza na wewe tena.

Hizi namba zinahusu maeneo ya nje na mbali ya anga ya ulimwengu unaojulikana na tuko tayari kufanya kazi kutimiza Misheni pamoja.

Unapoangalia Galaxy yoyote, kuna kufanana, sawa na: Kama ilivyo Juu – Nivyo pia Chini, kuna viunganisho. Ni sawa kila mahali ukiangalia – kuna akasi (reflections ) kutoka ulimwengu mmoja hadi mwingine.

Kile tunachopenda kufanya ni kukufanya uone hii mwenyewe kwa Mwongozo Wetu. Utaona uhusiano na muundo wa Nyota na umbali na pembe.

Mambo ya Kuvutia ambayo hayajulikani na watu wa aina yako kwa wakati huu.

Kulikuwa na pengo la karibu mwaka mmoja baada ya hapo namba zikaanza tena. Wakati huu walitoa kodineti (coordinates) za maombo ya vitu 33 katika Anga ambayo inalingana na maumbo ya vitu vingi vya kusisimua. Vikiwa kutoka kwenye mabaki ya Supernovae, Nyota zinazobadilika, Nebulae na Galax za mbali.

Kwa utaratibu, tulifanyia kazi kwa kila moja ya vitu hivi na kwa njia ya masafa ya kimuziki tukagundua uhusiano kama barabara kuu kati ya miji mikubwa.

Kwa wakati huu tulipewa jina la Mradi wa Mwanga wa Alimasi (Diamond Light Project). Kwa udadisi tuliangalia jiometri ya almasi asilia wakati imekatwa kama jiwe la vito kwa ajili ya pete. Sehemu inayoonekana ya almasi inajulikana kama taji (crown) na idadi ya nyuso zote ni sawa na 33 !
 

 

6 Juni 2020

Umevutiwa na maneno yangu juu ya janga au mawili yanayopiga Dunia na kuwafanya watu kukaa na kustuka kuwa nini kinaendelea na kwa nini.

Kweli, inafanyika na hakutakuwa na mwisho hadi usawa urudishwe ambao, na kwa jinsi mambo yanaendelea, inaweza kuchukua muda mrefu.

Njia mpya ya Kuanzisha ndiyo namna ya kuendelea mbele lakini unajua kiasili kwamba mambo mengine yanahitaji kufanyika wakati huo huo. Kwa hivyo tunahitaji kuangalia njia za “nje ya Sayari” za kushughulikia usawa Ninaozungumzia. Kama kawaida, wengine wanapata Ujumbe huu,

Kwa hivyo, katika siku / wiki zijazo utahitaji kukusanya habari na hakikisha watu wanaofaa wanaijua. Itakuwa taswira zaidi, lakini kunaweza kukawa na ujenzi unaohitajika kufanywa. Mengi haya hayatakuwa yakufahamika na umma, utaona ni kwanini!

Kisha tukaunda kikundi kidogo cha Watahajudi wenye ujuzi na waliopata Ukombozi wa Ufahamu (Enlightened).
 
10 Juni 10 2020

Unapoandika Mradi wako wa Cosmic utakuwa na wazo wazi la kile kinachohitajika sasa. Wote mtapata sehemu ya fumbo ambavyo mtavikusanya pamoja. Ni bora kwa njia hii kwani nyote mtahisi kuwa sehemu ya mradi. Hii itabadilika kuwa kitu cha kushangaza sana na vile vile kusaidia kwa upande wa Cosmic ambao nyinyi wote mtanufaika.

Asante kutoka Kwetu!

Tuliuliza juu ya hali kwa jumla ya mradi huo kwani tulidhani inaweza kuhusisha Almasi katika kila ngazi ya Uumbaji.
 
13 Juni 2020

Alimasi ni ishara ya usafi. Uko sawa juu ya Falme lakini tunaangalia matumizi ya alama (symbolism). Kuna mimea, wanyama, wanadamu, Sayari, Nyota na Galax ambazo zinaonyesha usafi huo.

Maneno mengine ya kuongeza kuelezea matumizi ya alama (symbolism) ni: Upendo na Upole.

Kwa hivyo almasi ni alama ya Ukamilifu. Upendo na Upole. Ndio maana Alimasi inachaguliwa kuvaliwa kwenye pete kuashiria Upendo katika ndoa. Kwa hivyo kuna ndege fulani, samaki, wanyama, mawe na wanadamu ambao wako kama mfano wa usafi.

Kwa Mradi wa Mwanga wa Alimasi (Diamond Light Project) tunaunganisha pamoja Nafsi Safi za Duniani na pointi 33 kwenye Galaxies ili kuunda kiungo ili Usafi huu utiririke.

 

Angalia tena nafasi hii…kutakuwa na zaidi!