Free Will

 

Kwa miaka mingi suala la ‟Free Will” limeulizwa mara nyingi na majibu tofauti yametolewa. Tunadhani baadhi ya hayo majibu yana mantiki kidogo sana. Kwa mfano: Kutoka kwenye ‟Enlightenment” kuna kitu kimoja kila mahali kwa hiyo hakuna pande mbili, hakuna uchaguzi hakuna ‟Free Will”. Hata hivyo, hii inaonyesha kwamba unaweza kuwa na mtazamo kutoka ‟Enlightenment” na akili pia ikiwpo kwenye ‟Enlightenment”. Hii ni wazi kuwa sio sahihi. Njia bora ya kuonyesha hii itakuwa: tangu kufikia ‟Enlightenment” mimi nimekuwa na ‟realizations” ambazo zimesababisha jinsi ambavyo sasa nafikiria ………

Maswali ni matokeo ya akili ambayo lazima pia kuwa mpokeaji wa majibu yoyote. Tunapaswa kuonyesha unyenyekevu na maarifa ya kawaida na kutambua kuwa chombo tunachotumia ingawa ni muhimu sana katika hali nyingi ni nje ya kina chake kabisa linapokuja suala la maswali makubwa. Kama Uongozi daima Wanavyotukumbusha “hutuna uwezekano wa kuanza kuelewa, ni ngumu sana kiakili.” Hiyo haitufanyi tuache kuendelea kuuliza maswali na kujenga mifano ya kiakili ya kusaidia kukidhi udadisi wetu. Kile ambacho tunatumaini ni kuwa, kinapaswa kuwa rahisi na kueleza matukio tuliyoona na kuwa “kweli” kwa mtazamo wetu huu mdogo.

Tumeambiwa kwamba tunachagua maisha yetu, kwa msaada wa Viongozi, ili kujifunza “mafunzo ya maisha”. Sababu ya mafunzo ni ili tuachilie “let go” labda ili tuweze kuishi zaidi katika ulimwengu wa Kiroho ambapo kujifunza kunaendelea. Kuhudumia inaonekana kunakwenda sambamba na kujifunza; zaidi tunavyojifunza, zaidi tunaweza kutoa. Maisha tunayochagua yanafaa, kimuundo, dhumuni au madhumuni tunayohitaji kwa masomo yaliochaguliwa wakati wa maisha wa mwili huo. Kama kawaida ya shule yoyote baadhi ya wanafunzi hushindwa, wengine hufikia malengo yao wakati wachache wanazidi matarajio yote.

Kwa mfano wa kulinganisha ni kama kuandika mchezo na kuucheza. Mpaka unapoanza kucheza sehemu yako na wachezaji wengine sehemu yao, kwa kweli huijui jinsi mchezo utakavyokuwa. Pengine unaweza kulazimika kuandika upya na kubadili baadhi ya maadishi ya mchezo! Kuna mambo mengi yasioyojulikana hasa kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wanaohusika na kwa sababu ya kutotabirika kwa ‟Free Will” zao. Mfano zaidi kama pakiti ya karata za kawaida za kucheza ambazo ma‟jokeri” huingizwa na kuchukua nafasi ya kadi yoyote ile kama “wild cards”. Ingawa unaweza kutabiri matokeo fulani mengine bila kabisa yatakushangaza.

Uongozi uliongeza:

Tuna furaha kuzungumza kuhusu jambo hili. Ni muhimu kwamba watu Wanaotahajudi wawe na mawazo fulani juu ya somo hilo kubwa.

“Je, tunawajibuka kwa makosa yetu au yangetokea tu bila kujali nini tunafanya?”

Hili ni swali huulizwa mara nyingi kwa namna moja au nyingine. Ili kujibu inahitaji kuangalia mtu anauliza swali kutoka wapi. Kama linaulizwa kutoka kwa mtu “aliyefungwa” katika dunia basi tunahitaji kujibu kutoka kiwango hicho. Kama linaulizwa kutoka kwa mtu anayetahajudi na kuhoji “free will” basi jibu litakuwa tofauti. Ni suala la mtazamo.

Kama mtu hupitia maisha yake bila kuhoji kamwe basi huzuni sana hutokea. Kamwe hawasimami na kuuliza swali hili la kina ambalo, wakati likijibiwa, na kueleweka kikamilifu linaweza kupunguza kiasi cha maumivu yao. Kwa mfano mimi peke ninawajibika kwa matendo yangu, Nina uhuru kwa hiyo naweza kuchagua njia yoyote ninayopenda kuchukua …… inaweza kusababisha …… ..Yote hii ni kosa langu kuwa imetokea! Kama nisingechagua kufanya hivyo! Nani ni ‟Mimi” kinachozungumza?

Uhuru au ‟Free Will” ni suala gumu kwa sababu, kama ulivyoonyesha sawa kuwa, binadamu kwa kawaida hujaribu kuelewa kwa akili zao ambazo ni wazi zina mipaka. Lakini kwa mtazamo finyu wenye mipaka inaweza kuonekana kuwa “mashine” ambayo inafanya kazi kwenye Ulimwengu huu ikishawekwa kwenye mwendo inakuwa na maisha ya peke yake, kwa kuwa, magurudumu yanazunguka na kunakuwa na utabiri fulani. Usiku na mchana, majira, mawimbi n.k. Lakini je umeangalia pia kwenye tabia za watu ambazo wamezaliwa nazo. Kuna utabiri fulani pia. Hivyo mtu huyo aliyezaliwa katika “tabia” hataweza kuwa na “free will” kwa maana ya uhuru kwa sababu yeye ni kama “mashine” tu.

Basi ni vipi kuhusu mtu aliyezaliwa na hali ya kutotabirika, kama ninyi. Je, unaweza kusema pia kwamba huna kuchagua au “free will”? Hapa matatizo huanza ………… Wakati Kiumbe kinaamua mwili gani wa kuchukua, akili gani na hisia gani za kuchukua, mahali pa kuishi nk. maisha yale yatafanyika chini ya mwavuli wa mtu huyo wa kutabirika. Kwa maneno mengine yeye ataitikia na ku ‟react” kwenye hali mbalimbali kama vile alivyopangwa ‟programmed” kufanya na aina hiyo ya mwili / akili / hisia nk.

Hata hivyo mfano wako wa Joker katika pakiti ya karata ni sawa kabisa. Katika kila maisha kuna “wild cards” zilizoweka katika mwili hivi kwamba kama watu wanataka, wanaweza kuvunja na kutoka nje ya “mould” na mipaka ya miili waliyochagua.