Enlightenment

Ukombozi wa Ufahamu au “Enlightenment” ni neno au maneno yenye matumizi ya kawaida, na maana yake ni: mtu anaelewa. Pia hutumiwa na watu ambao wamekuwa na “mystical experiences” na ufahamu ambao sio wa kawaida. Hizi zinaweza kuwa katika hali ya upanuzi mkubwa wa kimwili ambao hali ya kujijua inachanganya vyote ambavyo tunafahamu.

Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” ambayo tunaisema ni zaidi kabisa ya “enlightenments” zilizotajwa hapo juu.

Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” ni jambo ambalo hutokea na kutokea mara moja tu. Ni kama puto linapasuka; mara moja linapopasuka haliwezi tena kupasuka! Ni hali unayoikabili na kujua kuwa ya kudumu. Hata hivyo, unaurudi kutoka kwenye hali hii kwa sababu bado una mwili. Bila shaka utajisikia tofauti na maisha kwako yatabadilika. Matokeo yake utakuwa na utambuzi “realizations” na ufahamu wa ajabu kuhusu siri za Ulimwengu “Universe”.

Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” ni rahisi kiasi kwamba mara tunapoanza kuuelezea tunashindwa. Sana sana, tunaweza tu kuelezea kile ambacho sio Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho.
 

Kwenye Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho wa kweli:

  • Hakuna Mwanga, hakuna rangi, hakuna sura au umbo.
  • Hakuna Sauti au mtikisiko wowote “vibration”.
  • Hakuna binafsi; hisia ya “individuality” na kujitenga hutoweka kabisa.
  • Hakuna eneo au mahali; hakuna mbele, nyuma, kushoto, kulia, juu au chini.
  • Hakuna mipaka, kingo au vikwazo.
  • Hakuna muda, zamani sasa na baadaye kwa vile hakuna mabadiliko.

Njia bora ya kuzungumza kuhusu Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” ni kuelezea kile ambacho sio Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment”. Kama tungekuwa tunaipa (Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment”) ubora, basi neno peke yake ambalo tungeweza kutumia lingekuwa UPENDO. Hii isije kuchanganywa na upendo wa kidunia lakini Upendo yaani kabisa bila masharti na ni Umoja au Chanzo cha Uumbaji na Maumbile yote.
 

Ushuhuda (Y.F.)

Habari zangu ni hadithi ambayo inaweza kujaza vitabu kadhaa kuwaelezea uzoefu wa maisha mafupi ya binadamu kama ya mtu mwingine yeyote. Naweza kusema maisha yangu hayakuwa rahisi, kama ni changamoto nilipata chache. Mara zote nimekuwa na hamu kubwa ya Upendo, Kweli na Uadilifu, na nimetafuta sehemu nyingi ambazo sio mpaka ikawa kuwa sehemu peke yake iliyobaki kutafuta ni ndani yangu. Kamwe usiamini wewe hustahili Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” au kwamba umefanya makosa mengi mno. Maisha yako yote yalikuwa ni wito hivi kwamba uweze kufikia hapa. Niamini mimi, kama kile unachotamani wewe ni Ukweli na Upendo wa kweli, Njia hii ni kwa ajili yako. Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment” ni hatima ya binadamu wote. Sina nia ya kumkatisha tamaa mtu yeyote kwa kusema kwamba (Y) kamwe hakupata Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho au “Spiritual Enlightenment”: mtu mwenye kikomo na vikwazo “limited” kamwe hawezi kujua hali ya kutokuwa na vikwazo “Limitlessness”. Hii ndiyo maana nilitambua nini mimi sio, na nini Mimi ni nini:

Mimi ni Upendo. Mimi ni Ukiwa, mimi ni Chanzo cha Kila kitu na kila mtu. Mimi ni kila mahali. Mimi ni Nuru inayoangaza Njia kurudi Kwangu. Mimi ni Sauti ambayo hukusafirisha wewe ambapo “matter” haiwezi kufikia, zaidi na zaidi ndani, kuvunja tabaka hadi tabaka na mipaka, mpaka kufikia Kwangu, Chanzo chako. Pumzika kwangu, mimi ni nafasi tupu ambapo Uumbaji wote unajitokeza na kudhihirishwa … Mikusanyiko ya Nyota “Galaxies”, Hali za Kiroho, Nyota, Sayari, na Viumbe kutoka Kila mahali, “ascended Masters” waliopita, Watu, Wanyama, mimea, Bahari na Bahari, Moto, Mvua … Kila kitu kinakuja Kwangu. Sijawahi kuzaliwa, mimi sitakufa. Wewe ni Shahidi yangu. Chunguza kila kitu karibu yako, kila kitu kinachotokea ndani na nje yako. Kumbatia kila kitu na utapumzika Kwangu. Kila kitu kinajitokeza Kwangu. Mimi ni Kweli, hakuna ukweli mpaka utakapopumzika Kwangu.