Fanya Enlightenment iwe lengo lako: Ndiyo Sababu ya Wewe Kuwepo


“Nilichukuliwa kwenye ngazi mbali mbali za Mwanga ambazo zilifunua maumbo yaliyo na uzuri usiyoweza kuelezeka na Ukamilifu kabisa usio na kiasi wala mipaka. Hisia zangu zilizidiwa na mara moja akili yangu ilijiona jinsi ambavyo sio kitu. Upendo nilioshuhudia siku ile ulibadilisha maisha yangu milele; sikuwa na kingine cha kufanya isipokuwa kulia!”
(soma zaidi)

 

 

Mara tunapochukua miili yetu moja kwa moja tunajikuta tumewekwa kwenye mipaka. Ile mipaka sio ya nje tu; wengi wetu hatuna habari au hatujui ngazi mbali mbali nzuri za Ufahamu, nyingi na kubwa mno zilizoko ndani mwetu.

Baadhi ya watu wameweza kuona kidogo tu, na wengine zaidi kwa ajili ya unyeti wa asili.

Kwa hiyo, lengo la hii Tahajudi ya Mwanga na Sauti “Light and Sound Meditation” ni kumsaidia yeyote ambaye yuko tayari kutumia na kutenga saa moja kila siku, kuweza kuingia kwenye maeneo haya yanayotia moyo. Ni Safari ya Mwisho ya uvumbuzi ambayo itakupa haswa sababu ya kweli ya maisha yako.

Tovuti hii nia yake ni kumfikia kila mtu, yule ambaye ndio kwanza anaanza, mpaka wale ambao wameshajaribu “Meditation” lakini wakashindwa kufikia lengo lao la Kiroho. Bila kujali imani za kidini na falsafa, sisi tunakaribisha watu kukubali uongozi wetu ili waweze kujua Chanzo cha Kuwepo kwao kwa ku“Resonate” na Mwanga na Sauti ya Mungu.

Njia hii mpya ilianzishwa na kikundi kidogo cha watu ambao wamepata Ukombozi Wa Ufahamu “Enlightenment” ya Kiroho kwa kutumia tahajudi “Meditation” ya Mwanga na Sauti. Tulipata mawasiliano mnamo tarehe 16 Februari 2015 kutoka kwa “Intelligence” ambayo kihistoria inajulikana kama “Uongozi Wa Kiroho” na wito wa kufanya “Nguvu za Kimungu” ziweze kupatikana kwa watu wote ili kutoa nafasi kwa wale ambao hasa wanatafuta waweze kufikia Hali hiyo ya Ufahamu kama sisi wenyewe. Hatuna kiongozi; kila mmoja wa Walimu wetu anafanya kazi “autonomously” mwenyewe. Tunachoomba tu ni kwamba watu waweze kuambatana na kanuni za kimsingi zinazoonekana hapa chini. Kwa kutumia njia hii tunatarajia kuepuka matatizo mengi ambayo huonekana kuwa pigo kubwa kwa mashirika na makundi ambayo mara nyingi hupoteza Lengo la Kweli la Kiroho. Kwa habari zaidi kuhusu Uongozi wa Kiroho: Bofya Hapa kwenda kwenye tovuti ya “Utawala Wa Kiroho”.


Ina taarifa ambayo inahusu historia yao, sababu ya Wao kufanya mawasiliano sasa, madhumuni ya “Tahajudi” ya Mwanga na Sauti na taarifa zao zote za hivi karibuni. Wao wanazungumzia kuongeza Ufahamu wa Dunia na wakazi wake – mabadiliko makubwa. Tafadhali kumbuka: taarifa zote kutoka “Uongozi Ya Kiroho” zimeandikwa katika rangi ya Magenta.

Uongozi Wa Kiroho Wametuma ujumbe ufuatao:-

Kutokea hapa tulipokaa sisi, kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, imekuwa muhimu kuleta chini kiasi kikubwa cha Nguvu ya kushughulikia kukosekana kwa usawa wa dunia. Kuna wengi wenu tayari wanasaidia katika kazi hii. Tunachoomba ni kuwa watu waangalie mioyoni mwao na kuleta mabadiliko makubwa kwa kushughulikia masuala matatu makubwa:

KUKUBALIKA, UPENDO, MSAMAHA

Kwa masuala hayo matatu yakiwa muhimu kwenye akili za watu dunia yenu itasaidiwa mno kuzidi kipimo chochote kile.

 
mantra meditation
 

Baada ya kupokea habari hizi tulikuwa katika mshangao kwa Huruma Waliyo onyesha na kuona jinsi tulivyo heshimiwa tukaamua kufanya kile tunachoweza kwa upande wetu ili kuwasaidia watu kuwa na ufahamu wa Nguvu hizi. Tunaahidi, kwa kadri ya uwezo wetu kuhudumia hiki “Chanzo Cha Mwisho” hadi mwisho wa maisha yetu duniani.

Hakuna sheria za jinsi ya kuishi maisha au shirika rasmi; hatutarajii imani, ila uaminifu na muda ili tuweze kuthibitisha tunachodai. Hakuna wajibu wowote wa fedha kwetu kwa njia yoyote ile: unaweza kupenda kusoma sehemu kuhusu Kutoa katika ukurasa Maisha, inayoelezea jinsi sisi wote tunavyoweza kuchangia kwa dunia kuwa bora na kupendekeza Tahajudi ya Mwanga na Sauti ya Kiroho ambayo ni Upendo katika hali yake ya juu.
 

Watu Wanasikia Sauti ya juu “High Frequency Sound”

Watu wengi duniani kote, wamekuwa na ufahamu wa sauti ya juu ambayo haionekani kuwa na asili ya kimwili!

Tunaelewa kwamba Ulimwengu “Universe”, kama wanavyosema wanasayansi, ni mkusanyiko wa nguvu; kila nguvu ikiwa na tabia na kasi yake ya mzunguko.

Wakati tunapopokea “Divine Spark”, kwa njia ya kuguswa na mtu ambaye ana Ukombozi wa Ufahamu “Enlightened person”, tunakuwa na ufahamu wa Nguvu za Vipimo vya Juu ambavyo awali vilikuwa siri kwetu. Zinaelezeka kama Mwanga na Sauti kama vile tunavyohisi mwanga na sauti kwa hisia zetu.

Hata hivyo hizi nguvu za Kiroho hazionekani kwa njia hiyo. Ni kana kwamba tumepewa seti nyingine ya macho na seti nyingine ya masikio zinazofanya kazi kabisa huru bila kutegemea macho na masikio yetu. Kwa hiyo inawezekana kufahamu sauti ya mwili ya kawaida na Sauti ya Kiroho wakati huo huo!

Jinsi ambavyo watu zaidi wanavyo kuwa na ufahamu wa Nguvu za Juu inafanya kuwa rahisi kwa wengine kuifuata na kuifahamu na hii imesababisha jambo hili la kuvutia kutokea. Watu wengi (japo sio watahajudi) kote duniani wametoa taarifa kwamba wanasikia sauti ya juu.

Wanasema inasikika na kutoweka muda wowote ule bila kutegemea “randomly”. Inaweza kujitokeza wakati wa utulivu na wakati mwingine hata kama kuna kelele nyingi. Wanaielezea kwa ujumla kuwa nzuri na hata kutia faraja. Walipoulizwa kuelezea watu hao kwa kawaida husema ni kama mchanganyiko wa sauti za juu za asili.

Tunaambiwa kwamba hiki ni kipengele cha Sauti ya Kiroho ambayo inaweza kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia Tahajudi ya hali ya juu. Cha kusisimua ni kwamba inawaelekeza watu kwenye mwelekeo ambao awali walikuwa hawajui. Ni kitu cha “kutuamsha”.

Ukisikia sauti hii na unataka kugundua chanzo wake basi unahitaji kutafuta Kuanzishwa “Initiation” ya kweli ya Mwanga na Sauti. Tafadhali tuandikie na kutuambia kuhusu uzoefu wako kwa kutumia Ukurasa wa Mawasiliano. Tunaweza kujaribu kutafuta njia ya kudhihirisha na kukufunulia hizi Nguvu za Kiroho. Ukitaka kuchunguza jambo hili zaidi andika “Sauti ja Juu ya Kiroho” kwenye google, kuna habari tele ya wewe kusoma.
Kwa habari zaidi kuhusu Sauti ya Kiroho: (Bofya Hapa)
 

Tovuti ya Uamsho na Enlightenment

Kuna watu wengi ulimwenguni kote ambao bila kutarajia wanapata “Uamsho” na kusikia Sauti na / au kuona Mwanga wa Kiroho.

Kwa sababu hii tuliamua kutengeneza tovuti mpya ili kuwasaidia watu kuelewa kile wanakiona au kusikia na kutoa mwongozo ikiwa wanataka kutafuta Upanukaji zaidi wa Ufahamu.

Tunakadiria kuwa kuna mamilioni ya watu ambao wanaanza kuwa na ufahamu wa nguvu za Kiroho. Ikiwa unajua mtu ambaye unadhani anaweza kuwa katika kitengo hiki, tafadhali mtumie tovuti hii.
www.awakeningandenlightenment.com

 

Video ya YouTube ya Kiingereza hapo chini inaeleza muhtasari wa tovuti hii. Inaelezea namna mbalimbali za Uamsho na inatoa mwongozo kwa wale wanaotaka kufwata Njia Ya Kiroho.

 


 

 

Tahajudi Kwa Dunia Yote

Kama sehemu ya hoja ya jumla kuelekea kuwajali wengine tungependa Tahajudi mara kwa mara kufanyika kila wiki. Kwa wote kuwa pamoja kwa muda wa dakika 10 kwa wakati mmoja. Hii itakuwa taarifa ya nguvu kutoka kwenu kuthibitisha ukubali wenu kwa Sayari kwa ujumla. Katika kufanya hivyo mtahisi uhusiano mkubwa kati yenu .

 
mantra meditation
 

Idadi yetu imeongezeka kwa kasi cha ajabu katika kipindi cha miezi michache iliyopita, sasa ni zaidi ya watu 200 waliofikia Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho.

Lengo letu ni aina mbili, kwa Watahajudi kufikia Hali za Kiroho na kuongeza ufahamu wa Sayari. Kama sasa tuna kundi kubwa la watu walioanzishwa katika Nuru na Sauti ni wakati wa kuunganisha uwezo huu na kuandaa Tahajudi za pamoja dunia nzima.

Sisi ni tunapendekeza kwamba hii ifanyike kila mwishoni mwa wiki. Awali, kutuma Upendo na Amani kwa Sayari na wakazi wake kwa muda wa dakika 10. Ukitaka kuongeza wakati huu hiyo ni sawa lakini hakikisha kuanza wakati sahihi kwa eneo lako wakati. Angalia Tovuti ya Uongozi wa Kiroho.

Ingawa hili ni lengo la wale walioanzishwa kwenye Mwanga na Sauti tunawakaribisha watahajudi wote duniani wajiunge nasi kwenye lengo letu. Wengi wetu tunataka mabadiliko – hatimaye tuna uwezo wa kukamilisha hili – hebu tutumie vizuri fursa hii ya ajabu.
 
 

Kwa Muhtasari, Kanuni zetu ni kama ifuatavyo:

  • Hatuna Kiongozi, Walimu wetu wote wa Kiroho wanafanya kazi huru “autonomously”.
  • Sisi tunajitolea kusaidia watu wote ambao wanataka kugundua Hali hizi za Ufahamu wa Kiroho kwa kupitia Tahajudi ya Mwanga na Sauti.
  • Nguvu ya Mwanga na Sauti za kutahajudi hutolewa kwa kupitia Viumbe wa Uongozi wa Kiroho.
  • Hakuna mahitaji ya kimaisha, ila mapendekezo tu kwa kutumia akili na maarifa ya kawaida.
  • Hakuna ada yoyote, aidha kwa Mantras, Hali au Ufahamu wa Kiroho, au kwa mtu yeyote au shirika. Tunatumia kanuni ya “Lipa Mbeleni”.
  • Nguvu ya Mwanga na Sauti kwa ajili ya kutahajudi na ugunduzi wa Hali na Ufahamu wa Kiroho, inapatikana kwa watu wote katika nchi zote, bila kujali jinsia, hali, utamaduni, jamii au imani.
  • Watu wakichagua kutahajudi kwa nishati ya Mwanga na Sauti wana uwezo wa kuendelea kwa kiwango chao wenyewe.

 

Makala mapya zaidi kuhusu Kutahajudi kutumia Mwanga na Sauti itaonekana kwenye ukurasa wa Msukumo , hivyo usisahau kuuangalia. Tafadhali usisite kuwasiliana na sisi kwa maswali yoyote unaweza kuwa nayo kuhusu Tahajudi hii ya Nuru na Sauti, au taarifa yoyote juu ya Kiroho kwa kuandika kwenye  ukurasa wa Mawasiliano  wa tovuti hii.
 

Athari Nzuri ya Kuanzishwa “Initiations” kwa Sayari Yetu

Yote ni kwa sababu ya Upendo. Tunahitaji zaidi Upendo kwenye Sayari ya Dunia. Kuna chuki na kugombana sana kama tulivyosema; lakini kama kuna Upendo zaidi chuki itaondoka.

Tunataka watu ambao Wameanzishwa “Initiated” kukusanyika pamoja wakati mliokubaliana na kutuma Nguvu Ya Upendo kote Duniani. Baada ya kipindi hiki cha “Neema” kutakuwa na watu zaidi, hivyo ni lazima kuhakikisha kwamba hili linatokea.

Kuhusu Dunia yenyewe – ndiyo, inaumwa kama mgonjwa kwa sababu ya kile ambacho Binadamu amefanya kwa wanyama, misitu, mimea na yeye mwenyewe. Jinsi gani dunia itakabiliana na uharibifu huu wa makusudi? Inapaswa kushughulikiwa.

Kwa maelfu ya watu ambao watakuwa wameanzishwa “Initiated”, tunatarajia watakuwa hai kwa kuwa na mijadala kuhusu hofu yao juu ya matendo hayo. Kisha hatua kwa hatua watu wanaofanya mambo haya watasimamishwa, au watajua kuwa hawawezi kuendelea kwa njia hii. Wakiwa nao uwezo na nguvu ya Kuanzishwa “Initiation” pamoja nao, watu watakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko kwa pamoja.

Sisi tunangalia na kupongeza kazi yote inayofanyika ya watu kujiandaa kwa ajili ya uzinduzi wa Kuanzishwa.

Huu ni mwanzo wa wimbi kubwa la Nguvu Duniani kote, ambalo halijawahi kuonekana kwa muda mrefu. Tunaona nyie kama aina ya Nguvu ambayo hivi karibuni zitawashwa, na kutumia mwanga na nuru yenu kumulika Dunia.

 
mantra meditation
 

Kwa wale Wanaotafuta Kuanzishwa “Initiation”

Huu ni ujumbe kwa wote ambao wanataka Kuanzishwa “Initiation”, kupata Ufahamu wa ngazi za juu zaidi au kuendeleo kwenda kwenye Njia ya Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho “Enlightenment”.

Sisi hapa tunaona maandalizi mengi yanayo endelea na inatupa moyo kwa sababu ina maana kwamba Nguvu zitakazotumwa zitatumika vizuri, na kwa dhamira inavyostahili.

Nyie, kama watu mnaotaka Kuanzishwa “Initiation” muwe na uhakika kwamba katika kila hatua ya Safari yenu ya Kiroho, Sisi tutawatunza, tutawasaidia na Kuwapenda.

Ni Safari ya kujua kuhusu maswali makubwa ambayo unaweza kuwa unatafuta kwenye maisha yako yote. Kwa mfano, “Kwa nini tuko hapa?”
Labda utakuwa umetafuta majibu katika vitabu vya kiroho na kukatishwa tamaa.

Kwenye hii Safari ya Mwanga na Sauti utapata majibu mwenyewe. Hakutakuwa na haja ya ufafanuzi kwani wewe mwenyewe utajua katika moyo wako kuwa majibu ni kweli; Yote hii itakuwa na maana kwako wewe.

Unaweza kugundua kuwa unafikiria kwa njia tofauti, mawazo ya zamani na jinsi ulivyokuwa, chakula, nk. vitabadilika. Hii yote ni utaratibu wa kawaida wa “kuachia” na kuwa na uwezo wa kuwa bora, kama unavyoweza kuwa wakati uko kwenye mwili. Kufikia hali ya juu kabisa ya Ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho “Enlightenment” – ambayo, nayo itasaidia kuongeza uelewa wa binadamu wenzio.

 

Mawasiliano

Tunajua kuna wengi wenu duniani kote, ambao mnavutiwa na mnachokisoma. Tafadhali jitambulisheni kwetu, hasa wale wanaotafuta Kuanzishwa kwenye Mwanga na Sauti “Initiation”. Tafadhali jisikie huru kuuliza maswali yoyote uliyonayo kuhusu kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti au taarifa kuhusu Elimu ya Kiroho kupitia Ukurasa wa Mawasiliano wa Kutahajudi.

Upendo wetu kwenu wote.

 

Vipindi vya Neema “Grace”

Wakati Njia hii ilipoanza mnamo mwaka 2015 Uongozi wa Kiroho Walichagua nyakati maalum katika mwaka za kuongeza ukubwa wa Nguvu ya WimbiMwanga ‟Lightwave”. Hii iliwaruhusu Watahajudi nafasi ya kuendelea kwa urahisi zaidi na kupata Hali za juu za Ufahamu. Hata hivyo siku hizi kiwango cha Nguvu ni cha juu mno kiasi kwamba tuko kwenye kipindi cha Neema muda wote.

Hii imedhihirishwa kwa uwazi jinsi ambavyo Watahajudi wanasonga mbele haraka kwenye Njia ya tahajudi na kwa watu duniani kote kusikia Sound na kuona Mwanga wa Mungu bila kutegemea!

Hii, tunaambiwa, haijawawi kutokea kabisa. Tunashuhudia mwazo wa Kipindi cha ajabu cha Kiroho.

 

Tunamshukuru Amanda Sage kwa ruhusa ya kutumia picha yake ya Limbic Resonance.
www.amandasage.com